Skip to main content

MWIGULU NCHEMBA KUBARIKI TAMASHA LA KUIBUA VIPAJI VYA WASANII J'MOSI@STAR LIGHT HOTEL


Na Mwandishi Wetu

NAIBU  Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Mwingulu Mchemba (pichani) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la kuibua vipaji kwa wasanii chipukizi litakalofanyika Jumamosi kwenye ukumbi wa StarLight, Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Caasim Taalib akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana alisema tamasha hilo lenye ujumbe wa kuendeleza amani na Utulivu nchini litashirikisha wasanii zaidi ya 300 kutoka vikundi 20.

Alisema  SHIWATA inawakutanisha wasanii wa fani ya Maigizo, Filamu, Muziki wa Dansi, Bongo Flava, Taarab, Sarakasi, Karate, Judo, Taekwondo, Ngoma, Ngonjera, Mieleka, Gospel,Kasda,Kwaya, Mitindo ya Mavazi, Wachoraji na Wachongaji. 
Alisema mtandao wa SHIWATA wenye wanachama zaidi ya 7,000 nchini kutoka makundi ya wasanii, waandishi wa habari za Michezo na vijana imekuwa ukibuni njia mbalimbali za kuibua vipaji vya wanachama wake.

Mwenyekiti Taalib alisema tamasha la kwanza kama hilo lilifanyioka Agosti, 2012 katika uwanja wa Chuo cha Bandari Tanzania, Tandika Dar es Salaam ambako wanamichezo mbalimbali walishiriki. 
Wasanii walishiriki kuonesha sanaa zao ni mabondia ambao waliopambana katika uzani wa juu, muziki wa mchiriku, mpira wa mikono kwa ngongoti, mbio za farasi,mchezo wa mbwa kuruka moto na mchezo wa soka. 
Baada ya tamasha hilo SHIWATA imeandaa tamasha jingine litakalokuwa linafanyika kila mwezi katika kumbi mbalimbali na mikoani.

Katibu wa SHIWATA, Selemani Pembe alisema maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika na wasanii wanajifua kuja kuonesha uwezo wao jukwaani.

Mwimbaji wa kikundi cha taarab cha Super Shine Taarab, Queen Salma alisema wataonesha maana ya taarab na jinsi inavyochezwa jukwaani.

Comments