Tenas Aswile, mratibu wa tukio
ZAIDI ya mawakala 15 tayari wamewasiliana na Kampuni ya
Tanzania Mwandi kuwahitaji wachezaji mbalimbali kwaajili ya kuwapeleka kwenye
klabu za barani Ulaya, Asia na Afrika ili
kucheza soka la kulipwa.
Mwitikio huo umeongezeka kutokana na vijana wa kiafrika kuwa
na soko kubwa katika ulimwengu wa sasa wa mpira wa miguu kwa nchi mbalimbali
kama Sweden, Uholanzi, Denmark, Ureno na nchi nyinginezo.
Arne Anderson kutoka AA Football Service ya Sweden amesema kuwa binafsi yuko tayari kuchukua
wachezaji wawili kwaajili ya kuwatafutia clubs nchini humo kwani tayari
mafanikio ya wachezaji watano wa kiafrika aliowapeleka yamempa maombi ya timu
nyingi za Sweden .
“Niko tayari kuchukua wachezaji wawili endapo tutakubaliana
kuhusu maslahi yangu pindi wachezaji hao wakianza kucheza hapa”, Arne amesema.
Kutokana na mafanikio hayo na maombi ya mawakala lukuki
Kampuni ya Tanzania Mwandi inazidi kuwasisitizia wachezaji wa Kitanzania kujaza
fomu zinazopatikana kupitia blog.tanzaniamwandi.co.tz ili kufanya majaribio ya
kucheza soka nchini Sweden, Norway, Denmark, Uholanzi, Ureno, Uswiss, Ufaransa
na Ubelgiji, barani Asia (Kuwait, China, Qatar nk) na klabu nyingine barani
Afrika.
Mpaka sasa jumla ya wachezaji wa kitanzania 15
wamekwishajaza fomu za haraka kwenye tovuti ya Tanzania Mwandi huku kampuni
ikiwa imepokea pia maombi ya wachezaji 25 kutoka nje ya nchi.
“Maombi yanazidi kuja ingawa tunawahimiza Watanzania wasikimbie
kiingilio cha shilingi 300, 000 wakumbuke kuwa wanafanya majaribio wakiwa
nyumbani na watakapopata timu Kampuni ya Tanzania Mwandi haitachukua chochote
kwenye mikataba yao ,
ni wao na mawakala ndio watakokubaliana juu ya watakachokipata kutoka kwa klabu
husika”, alisema Teonas Aswile, Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzania Mwandi,
waandaaji wa African Youth Football Tournament.
Aswile amezialika klabu mbalimbali za ligi kuu ya soka
Tanzania Bara na Visiwani kutazama wachezaji watakaofika katika michuano hiyo
kwani wapo baadhi ya wachezaji kutoka nje ya nchi ambao watafika na wangependa
kucheza soka la Tanzania .
“Kati ya wachezaji 25 wa nje ya nchi wengine wameomba
tuwatafutie timu hapa nchini hivyo klabu zikija zinaweza kuwapata wachezaji hao
wakiwa huru kwasababu watakuja kwa gharama zao kufanya majaribio nchini. Pia
klabu hizo zitumie fursa hii kuuza wachezaji wake.”
Michuano ya African Youth Football Tournament inatarajia
kufanyika Juni 10 hadi 14 mwaka huu katika uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam na kushirikisha vijana kati ya miaka 18 hadi
21 kutoka Tanzania
na bara zima la Afrika. Taarifa zaidi kuhusu michuano hiyo zinapatikana
kupitia; blog.tanzaniamwandi.co.tz
Comments
Post a Comment