FFU NGOMA BAND NA SALAMU ZA MEI MOSI


Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa band" aka FFU
yenye makao kule Ujerumani,inawatakiwa kila la heri na fanaka wadau wote
katika kusherehekea siku kuu ya wafanyakazi duniani "Mei Mosi" (1st May).

Pongezi kwa Wafanyakazi wa sekta zote kuanzia wachuuzi,akina mama nitilie,
wafanyakazi viwandani,maofisini,mashambani,wapagazi,wakokota mikokoteni n.k, Kazi ni kazi ! 
Baada ya kazi tufurahie Mei Mosi kwa kupata burudani kamili ya muziki kama vile
"Bongo Tambarare" na Supu ya mawe, n.k at FFU camp