AZAM FC YAZIDI KUIKABA KOO YANGA SC


AZAM FC jana walizidi kuichimbia kaburi la kushuka daraja, African Lyon baada ya kuilaza mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliopigwa dimba la Chamazi Complex, Mbagala jijini Dar es Salaam, 
Mcha  Khamis Mcha ‘Viali’,  Kipre Tchetche ambaye alifunga mawili, huku lile la Lyon lilifungwa na Adam Kigwande 
Kwa ushindi huo, Azam imezidi kuwafukuzia vinara wa ligi hiyo Yanga wenye pointi 49, baada ya kufikisha pointi 46, lakini ipo mbele mchezo mmoja.
Kwa upande wa Lyon, imezidi kuchungulia daraja la kwanza, ikibakia na pointi zake 19 baada ya kushuka dimbani mara 23 ikiwa nafasi ya pili kutoka mkiani.
Mara baada ya filimbi ya mwisho ya mwamuzi, Godfrey Tumaini, Kocha wa Lyon, Charles Otieno, alijitosa uwanjani kumvaa akidai kuipendelea Azam, lakini Polisi walimdhibiti na kumtoa nje ya uwanja.