YANGA YAJIWEKA TAYARI KUWAVAA MAAFANDE WA MORO J'MOSI



Kikosi cha Young Africans Sports Club
Baada ya kuichapa timu ya Ruvu Shooting kwa bao 1-0 katika mchezo uliopita mwishoni wa wiki na kuwa ushindi wa tano mfululizo, Young Africans Sports Club itashuka dimbani siku ya jumamosi kucheza na timu ya Polisi Morogoro yenye makao yake mjini Morogoro , mchezo utakaofanyika katika dimba la Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kuanzia majira ya saa 10 jioni. 
Young Africans ambayo inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa kuwa na pointi 48, mabao 37 ya kufunga na mabao 12 ya kufungwa, iko mbele kwa pointi 11 zaidi ya timu ya Azam inayoshika nafasi ya pili kwa kuwa na ponti 37 na mabao 32 ya kufunga na mabao 16 ya kufungwa.
Mara baada ya kupata ushindi wa tano mfululizo katika michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom, kikosi cha mholanzi Ernie Brandts kimeendelea na mazoezi katika uwanja wa mabatini Kijitonyama siku ya leo ikiwa ni sehemu ya maandalzi ya mchezo wa siku ya jumamosi.
Katika mchezo wa mwisho Young Africans iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya  Ruvu Shooting bao lililofungwa na mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Uganda Hamis Kiiza, tangu mzunguko wa pili uanze Yanga imeshacheza jumla ya michezo saba na kufanikiwa kushinda michezo sita na kutoka sare mmoja hivyo kujikusanyia pointi 19 kati ya 21.
Ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa Ubingwa, Kocha Mkuu Brandts amesema anakianadaa kikosi chake kuhakikisha kinapata pointi 3 katika kila mchezo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa Ubingwa.
Akiongea na www.youngafricans.co.tz leo asubuhi mara ya baada ua mazoezi, kocha mkuu Brandts amesema anajua mchezo dhidi ya timu ya Polisi Morogoro utakua mgumu, kwani timu ya Polisi itapigana kuhakikisha inapata pointi ili iweze kujinasua katika msitari wa kushuka daraja, kila mchezo tunaocheza kwa sasa ni fainali kwetu.
 
Wachezaji walifanya na mazoezi leo ni :
 
Said Mohamed, Yusuph Abdul na Ally Mustafa 'Barthez' (magolikipa) 
Kelvin Yondani, Nadir Haroub 'Cannavaro', Shadrack Nsajigwa, Stephano Mwasika, Salum Telela, Oscar Joshua, Godfrey Taita na Juma Abdul (walinzi)
 Frank Domayo, Saimon Msuva, Nurdin Bakari, Omega Seme na David Luhende, Reheni Kibingu, (viungo) 
 
Hamis Kiiza, Jerson Tegete, George Banda, Nizar Khalfani, Didier Kavumbagu na Said Bahanuzi (washambuliaji) 

Mbuyu Twite na Haruna Niyonzima wataungana na wenzao kesho asbh kufuatia kuwa na matatizo tofauti yaliyowafanya washindwe kufanya mazoezi asubuhi ya leo.
CHANZO:www.Youngafricans.co.tz
 

Comments