Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Ruvu Shooting na Yanga
iliyochezwa jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 62,228,000
kutokana na watazamaji 10,929.
Viingilio katika mechi hiyo namba 146 iliyomalizika kwa
Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000
na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 14,336,764.95 wakati Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 9,492,406.78.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh.
7,289,880.48, tiketi sh. 4,136,390, gharama za mechi sh. 4,373,928.29, Kamati
ya Ligi sh. 4,373,928.29, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
2,186,964.14, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh. 850,486.06 na
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 850,486.06.
Comments
Post a Comment