Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeteua
waamuzi kutoka Angola kuchezesha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya
Tanzania (Taifa Stars) na Morocco (Lions of the Atlas).
Mechi hiyo ya kundi C itachezwa Machi 24 mwaka huu kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Ivory Coast ndiyo inayoongoza kundi hilo ikiwa
na pointi nne na kufuatiwa na Taifa Stars yenye pointi tatu.
Mwamuzi wa mechi hiyo ni Helder Martins de Carvalho wakati
mwamuzi msaidizi namba moja ni Inacio Manuel Candido huku Ricardo Daniel
Cachicumi akiwa mwamuzi msaidizi namba mbili. Mwamuzi wa mezani (fourth
official) ni Antonio Muachihuissa Caxala.
Waamuzi hao watawasili nchini saa 1.20 usiku Machi 22 mwaka huu
kwa ndege ya Kenya Airways wakitokea Luanda, Angola kupitia Nairobi, Kenya.
Kamishna wa mechi hiyo atakuwa David Fani kutoka Botswana
anatarajiwa kuwasili Machi 22 mwaka huu saa 1.45 usiku kwa ndege ya South
African Airways.
Naye mtathmini wa waamuzi (referee assessor) Neermal Boodhoo
kutoka Afrika Kusini atawasili nchini Machi 22 mwaka huu 1.45 usiku kwa ndege
ya South African Airways.
Comments
Post a Comment