Skip to main content

UKATA WAFANYA SHINDANO LA MISS UTALII KUPIGWA KALENDA


BAADHI YA WASHIRIKI WA MISS UTALII  TANZANIA, WAKIFUNDISHA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI BAGAMOYO, WALIPOTEMBELEA  SHULE HIYO

Fainali za Taifa za mashindano ya Miss Utalii Tanzania 2012/13, zilizo kuwa zimepangwa kufanyika 17,machi 2013  katika ukumbi wa Dar Live Dar es Salaam, zimesogezwa mbele hadi tarehe 30-3-2013,katika ukumbi utakao tangazwa badae. 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Rais wa Mashindano hayo nchini na Barani Afrika Erasto G., Chipungahelo, alisema kuwa sababu  ya kuahilishwa kwa fainali ni pamoja na upungufu wa bajeti ,uliosababishwa na baadhi ya wadhamini wakubwa walio ahidi kushindwa  kutimiza ahadi zao kama walivyo ahidi, hivyo kupelekea upungufu wa zaidi ya shilingi 170,000,000/= , kati ya bajeti ya shilingi 870,000,000/= zinazohitajika ili kukamilisha fainali hizo.

“Ili kulifanya shindano hili kwa ubora na kiwango cha kimataifa, tunahitaji sio chini ya shilingi 870 Milioni, ambapo hadi sasa tumefanikiwa kupata jumla ya shilingi 600Milioni, na tunaupungufu wa jumla ya shilingi 170 Milioni, ambao umesababishwa na baadhi ya wadhamini , kushindwa kutimiza ahadi zao kulikotokana na matatizo mbalimbali waliyo yapata ya kibiashara. Mashindano haya kama yalivyo mashindano mengine nchini na Duniani yanategemea udhamini kutoka kwa sekta binafsi na za umma, kwani gharama za kuyaendesha na kuyaandaa mashindano haya ni kubwa,ambazo haziwezi kulipwa wala kufidiwa kwa kutegemea viingilio vya getini”.
Hali hii imetulazimu kuahilisha fainali hizi hadi 30-3-2013,ili kupata muda wa kupata kiasi hicho cha fedha, na kukamilisha maandalizi kwa ubora na viwango vya kimataifa. Taratibu za kupata fedha hizo zinakaribia kukamilika kabla ya tarehe ya shindano kutoka kwa wadau wa utalii katika sekta binafsi na za umm. Kambi ya washiriki inaendelea katika hoteli ya Ikondelelo Lodge Dar es Salaam, ambapo kuanzia jumanne tarehe 19-3-2013 , washiriki wote wakiambatana na waandishi wa habari, wataanza ziara ya wiki moja katika hifadhi za Taifa za Mikumi,Saadani na Udzungwa, wakiwa katika hifadhi ya taifa ya Udizungwa washiriki watapanda milima ya udizungwa hadi katika kilele cha Maporomoko ya maji ya Sanje , ambayo ni kivutio kikubwa katika hifadhi hiyo.

Akizungumzia hali hii chipungahelo tumesikitishwa, na hali hii,tulijipanga na kujiandaa kwa makini,lakini bahati mabya mmoja wa wadhamini wetu amepata matatizo ya kibiashara,yote ni mipango ya mungu, na tunatambua kuwa washiriki wamekaa kambini kwa zaidi ya muda tulio kuwa tumeupanga,hivyo kutuongezea gharama, lakini baada ya kutafakari kwa kina tumeona kuliko kufanya shindano lililo chini ya kiwango, ni bora kuingia gharama zaidi za kambi ili tufanye shindano lenye hadhi na kiwango cha kimataifa na kuwa mfano kwa mashindano mengine nchini na Afrika kwa ujumla.Kwa washiriki ambao kwa sababu moja au nyingine hawatakuwa tayali kuendelea na kambi, basi milango iko wazi kwao na nafasi zao zitachukuliwa na washindi waliofuatia kutoka katika mikoa husika.

Sekta ya Utalii ni moja ya uti wa mgongo wa uchumi wa taifa,na sisi tunatangaza na kukuza utalii kitaifa na kimataifa,kwahiyo kwetu sisi ni ubora kwanza wa shindano na si bora shindano,bora hasara ya fedha kuliko hasara ya ubora wa shindano , ambalo ni alama ya urithi wa taifa.
Binafsi na kamati ya mashindano, hatutaki kuamini kuwa hii ni hujuma ,bali ni hali ambayo katika dunia ya biashara ya sasa, yeyote inaweza kumtokea, hivyo hatuna sababu ya kuchukua hatua za kisheria za kumshitaki mdhamini huyo, wala kumtaja katika vyombo vya habari,tumejiridhisha nae na kuamini bahati mbaya iliyo mtokea.

Tunawaahidi wadau na wapenzi wa mashindano haya kuwa dhamira,na nia ya kulifanya shindano hili kuendelea kuwa bora na lenye mafanikio makubwa kuliko jingine lolote nchini na Afrika iko pale pale, na hili litadhihirika hiyo siku ya tarehe 30-3-2013. Kwa wadau,wafanya biashara, makampuni binafsi na ya umma, hasa ya kizalendo tunaomba wajitokeze kutuunga mkono kwa kudhamini na kununua tiketi siku ya shindano. Kwa wale wasio tutakia mema basi wajiandae kuumbuka siku ya tarehe 30-3-2013.
Erasto G. Chipungahelo
Rais – Miss Tourism tanzania Organisation
 

Comments