TMK WANAUME FAMILY v TMK WANAUME HALISI KATIKA NANI MKALI SIKU YA PASAKA @ DAR LIVE

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). Kulia ni Meneja wa TMK Wanaume Family, Said Fella ‘Mkubwa’ na Meneja wa Wanaume Halisi, Abdallah Mashoto.
Mrisho akiteta jambo na Juma Nature na wenzake.
Wanaume Halisi wakiwa katika picha ya pamoja na meneja wao, Mashoto.
Wanaume Family wakiwa katika picha ya pamoja na meneja wao, Fella.
Juma Nature (kushoto) akiongea na waandishi wa habari.
Wasanii wa Wanaume Family, kutoka kushoto, Dogo Aslay, Stiko na YP wakiwa katika pozi.
Temba akiongea na waandishi wa habari.
Mhariri wa Gazeti la Risasi, Mohamed Kuyunga akiwa katika picha ya pamoja na Temba na Nature.
Temba akiingia kwenye gari lake tayari kwa kusepa.
Benjamin Mwanambuu, mmoja wa waratibu akiwa na Pamela Daffa, Mc wa dar Live.
Mashoto akitoa tambo zake.
Fella naye hakubaki nyuma, aliahidi makubwa.
Temba na wenzake wakisepa.
Ukumbi wa kisasa wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem, umeandaa mpambano wa kihistoria kati ya makundi mawili hasimu ya muziki wa kizazi kipya Bongo, TMK Wanaume Family na TMK Wanaume Halisi. Mpango mzima utatimua vumbi siku ya Pasaka na leo makundi hayo yalifanya mkutano na waandishi wa habari kwenye ofisi za Global Publishers, Bamaga jijini Dar.