WAKATI kikosi cha timu ya soka ya Taifa ‘Taifa
Stars’ kikiwa tayari kuivaa Morocco keshokutwa, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
limepiga marufu mashabiki kuingia ndani ya uzio wa uwanja.
Stars na Morocco zitakwaana kesho katika
uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mechi ya y Mchujo ya kuwania tiketi
ya kucheza fainali za kombe la dunia zitakazopigwa mwakani nchini Brazil.
Ofisa
habari wa TFF Boniface Wambura, alisema
kwamba wachezaji wote 23 walioitwa kwenye kikosi cha Stars wapo katika hali
nzuri na wanaendelea na mazoezi yao chini kocha mkuu Kim Poulsen.
Alisema kwa kiasi kikubwa kambi ya Stars iliyopo
kwenye Hoteli ya Tansoma katikati ya jiji la Dar es Salaam inaendelea vizuri huku
wachezaji wakiwa na ari kubwa ya kutaka kushinda mchezo huo utakaopigwa kuanzia
saa tisa alasiri.
Wachezaji wanaounda kikosi cha Stars ni pamoja
na makipa Juma Kaseja ambaye pia ndiye
nahodha wa Stars, Aishi Manula( Azam ), Hussein Shariff (Mtibwa Sugar) na
Mwadini Ally (Azam). Huku Mabeki ni
Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin
Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Nassoro Masoud Cholo (Simba) na Shomari
Kapombe (Simba).
Kwa upande wa Viungo ni Salum Abubakar (Azam),
Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha (Azam), Frank Domayo
(Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar). Wakati Washambuliaji
ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas Ulimwengu wa
TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Kuhusiana na Mashabiki watakaokiuka onyo la
TFF kwa kuingia kwenye uzio wa Uwanja wa Taifa, Wambura alisema mashabiki
watakaokiuka watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kufungiwa kuingia
katika uwanja huo.
Aidha, Wambura alisema kikosi kingine cha Morocco kilitarajiwa kuwasili jana tayari kwa
mchezo huo, ambapo kundi la kwanza lililowasili juzi na kufikia kwenye hoteli
ya Kilimanjaro Hyatt Regency ambapo leo
itafanya mazoezi yake ya mwisho kwenye Uwanja wa Taifa kuanzia saa 9 alasiri.
Kikosi cha Morocco kinachonolewa na kocha Kocha Rachid Taoussi kinaunnwa na
Nadir Lamyaghri, Anas Zniti, Yassine Bounou, Younnes Bellakhadar,
Abdellatif Noussair, Abderrahim Achchakir, Zoheir Feddal, Younnes Hammal,
Zakarya Bergdich na Abdeljalil Jbira.
Pia wamo Issam El Adou, Kamel Chafni,
Salaheddine Saidi, Mohamed Ali Bamaamar, Abdelaziz Barrada, Salaheddine Aqqal,
Abdessamad El Moubarky, Nordin Amrabat, Chahir Belghazouani, Abdelilah Hafidi,
Youssef Kaddioui, Brahim El Bahri, Hamza Abourazzouk na Youssef El Arabi.
Comments
Post a Comment