SINEMA ZA VIWANJANI BADO ZINAHITAJIKA KUFIKISHA TAARIFA ZA KIMAENDELEO

 Washiriki wa warsha ya kujadili na kuboresha mkakati wa Mawasiliano wa Wizara ya Fedha, kutoka vyombo vya Habari mbalimbali nchini wakijadiliana leo katika ukumbi wa Kilimanjaro Park Hotel, Kibaha mkoani Pwani.
 Kulia ni Othman Michuzi wa Mtaa kwa Mtaa Blog, akiwa na Dina Ismail wa Sports Lady Blog kushoto wakisikiliza kwa makini mjadala huo.

 Baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii wakiwa katika picha ya pamoja.(Picha kwa Hisani ya Mtaa kwa Mtaa Blog)



 Kushoto ni Thabit Matotola kutoka kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha na kulia Anthony Siame kutoka kampuni ya New Habari

Kulia ni Mahmoud Zubeiry wa Bin Zubeiry Blog akiwa na Henry Mdimu wa gazeti la Mwananchi na Ahmed Michuzi wa Jiachie Blog

Baadhi ya maofisa toka wizara mbalimbali nchini wakijadiliana katika warsha hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya Kilimanjaro Park iliyopo Misugusugu, Kibaha mkoani Pwani.


Na Sports Lady, Kibaha
IMEBAINIKA  kwamba bado kuna baadhi ya umuhimu wa kurejeshwa kwa vituo vya kijamii (Community Centres)  ili kuwezesha wananchi wote nchini kuweza kupata habari.
Hayo yalibainika mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa warsha ya siku moja kuhusu njia mbadala ya kufikisha taarifa za kimaendeleo kwa wananchi iliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na kushirikisha  wamiliki wa mitandao ya kijamii (Blogs), maofisa habari kutoka idara mbalimbali  na wadau wengine.
Wakichangia mada, wadau hao walidai kuwa licha ya kuwepo kwa utandawazi lakini kuna baadhi ya jamii na hasa za vijijini bado hazipati taarifa za matukio mbalimbali yanaoondelea katika ulimwengu huu.
Walisema hiyo inatokana na njia zinazotumika kutangaza hizo taarifa kutowafikia wengi kama inavyodhaniwa na hivyo bado kuna haja ya kurejeshwa vituo vya kupashana habari kama ilivyokuwa zamani.
“Sidhani huko vijijini kama kila mtu anauwezo wa kuliki simu ya mkononi au kuwa na uwezo wa kujiunga na mitandao ya kijamii, hivyo basi ni ngumu jamii hiyo kupokea taarifa mbalimbali za kimaendeleo hususani kama hizi za kibenki,”
“Zamani nakumbuka kulikuwa na siku na sehemu maalum watu wanakutana na kuangalia sinema mbalimbali kama ambazo zilikuwa ni maalum kwa kufikisha ujumbe fulani kwa jamii kama ukimwi n.k lakini hayo siku hizi hakuna, hivyo nadhani serikali ama mashirika yangetilia mkazo kurudisha mkakati huo,”waliongeza wadau hao
Wakienda mbali zaidi, wadau hao walisema kikwazo kingine ni lugha kwani kuna baadhi ya kampeni zinaendeshwa kwa lugha ya kiingereza kitua ambacho si wote wanaoifahamu kwa ufasaha lugha hiyo, pia kuna maeneo hata lugha ya Kiswahili hawaielewi zaidi ya lugha ya eneo husika hivyo ingekuwa bora hata kampeni hizo zikafikishwa maeneo hayo zikiwa katika lugha ya eneo husika. 
Awali, akifungua warsha hiyo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Kilimajaro Park iliyopo Misugusugu, Kibaha mkoani Pwani, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara  ya Fedha, Ingiahedi Mduma, alisema ni haki ya kila mwananchi kujua taarifa za kimaendeleo za nchi hivyo  wameamua kukaa chini na kutafuta njia mbadala ya kuiona ni jinsi gani taarifa hizo zitawafikia wananchi.

Comments