SHINDANO LA 'MORO CARNIVAL' MKOMBOZI WA VIJANA WENYE VIPAJI MJINI MOROGORO

 Kijana Mafuvu akionyesha umahili wake wa kucheza katika Shindano la Moro Carnival ambalo lilikuwa likiwapambanisha vijana wa mji wa Morogoro kuonyesha vipaji vyao mbali mbali. Shindano hilo lililofanyika katika uwanja wa Sabasaba mjini Morogoro, Moro Carnival lengo lake ni kuvumbua vipaji wa kuwashindanisha na kuviendeleza vipaji kwa vijana wa mji wa Morogoro. Vipaji vilivyokuwa vikitafutwa ni vya kudansi, kuimba, wasanii wa muziki wa Hip Hop, Uchekeshaji n.k.
 Watu waliojitokeza katika shindano hilo wakifuatatilia kwa makini mchuano.
 Majaji wa Shindano la Moro Carnival lililofanyika katika uwanja wa sabasaba, kutoka kulia ni Frado John, Msanii wa Muziki wa bongofleva Seleman Msindi 'Afande Sele', Wiliam Matajiri pamoja na mwanadada Adela Tilya.
 Jaji nambali moja Frado John akitoa makisi kwa mshiriki wa shindano la Moro Carnival.
 Jaji nambali mbili Seleman Msindi 'Afande Sele' akitoa makisi kwa mshiriki.
Mshiriki wa muziki wa hip hop, akionyesha makali yake ya kuchana wakati wa shindano la Shindano la Moro Carnival lililofanyika uwanja wa sabasaba mjini Morogoro.