SARE YAISHUSHA SIMBA SC, KAGERA SUGAR YAJINAFASI


Simba leo imelazimka kugawana pointi na wenyeji Toto African ya Mwanza baada ya sare ya mabao 2-2, katika mchezo uliopigwa Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza. 
Sare hiyo imeifanya Simba kushuka nafasi moja chini kutoka ya tatu   hadi ya nne kwani matokeo hayo yameifanya kufikisha pointi 34, baada ya jana Kagera Sugar kuwatandika mabao 2-1 ndugu zao, Mtibwa Sugar. 
Katika mchezo huo ambao ulitawaliwa na rafu za hapa na pale, Simba ambayo imeonekana kusuasua katika mechi zake za duru hilo la lala salama, ilionesha kiwango cha chini. 
Toto ndio walianza kuandika kalamu ya mabao katika dakika ya 24 kupitia kwa  Musa Said aliyepiga  shuti kali nje ya 18 na kutinga moja kwa moja nyavuni.Dakika tatu baadaye Said Mkopi aliisawazishia   Simba baada ya kuitendea  haki krosi ya Haruna Chanongo.Timu hizo zilikwenda mapumziko kwa sare ya bao 1-1.

Katika mchezo huo wachezaji wa Simba Jonas Mkude na Adam Miraji walilimwa kadi ya njano kwa kuwachezea vibaya wac hezaji wa Toito.

Dakikaya 36 Toto walishindwa kutumia nafasi nyingine waliyoipata kupitia kwa Evarist Maganga aliyeunganisha kwa kichwa mpira wa kona  uliopigwa na Emmanuel Swita na kutoka nje.

Dakika ya 40 Simba ilimtoa Jonas Mkude na kumuingiza Ramadhan Salum

Mshambuliaji wa Simba Mrisho Ngasa aliyeingia dakika ya 55 akichukua nafasi ya Mkopi aliwainua mashabini wa timu hiyo katika dakika yya 62 mara baada ya kufumua shuti kali nje ya 18.

Dakika ya 68 shabiki  wa Simba alikubali kichapo kutoka kwa shabiki wa Yanga mara baada ya kuzunguka uwanja na pikipiki akiwa na bendera na ndipo shabiki wea Yanga aliposhuka jukwaani na kuing’oa bendera  na shabiki huyo kushuka kwenye pikipiki na kwenda jukwaani ambapon alikumbana na kichapo hicho.

Selemani Kibuta aliisawazishia Toto dakika ya 72 baada ya mabeki wa Simba SC kujichanganya na kumpa mwanya mshambuliaji huyo wa Toto kufunga, aliyeingia kipindi cha pili kusawazisha.

Simba: Juma Kaseja, Nasoro Masoud ‘Cholo’, Miraj Adam, Shomari Kapombe, Hassan Khatib, Jonas Mkude, Amri Kiemba, Abdallah Seseme, Rashid Mkopi, Ramadhani Singano ‘Messi’, Haruna Chanongo.
Toto African:  Erick Ngwengwe, Erick Muliko, Robert Magadula, Evarist Maganga, Hamis Msafiri, Musa Msafiri, Emmanuel Swita, Henry Khalifa, James Magafu, Mohamed Jingo, Erick Kyaruzi.