RUSHA ATWAA TUZO YA SJMC MISS TOURISM TANZANIA 2012/13


Mshindi wa SMJC Miss Tourism Tanzania 2012/13 Media Award kutoka Mkoa wa Arusha Rose Godwin akivalishwa Skafu maalum ya ushindi na Mwalimu Mkuu wa Shule kuu ya Chuo Cha Uhandishi wa Habari SJMC, Drk. Herbert Makoye.

Fainali za Utalii Tanzania zimeendelea kushika kasi kwa warembo kushindania Tuzo mbalimbali za Utalii, Utamaduni, Jamii na za Kuichumi. Jana lilifanyika Shindano la kumpata Mshindi wa Tuzo   ya Habari (Media Award) , Shindano ambalo liloifanyika katika Viunga vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam , Shule kuu ya uandishi wa Habari na Mawasiliano ya umma (SJMC) ambao ni wadhamini wakuu wa Tuzo hiyo.
Katika Shindano hilo la Miss Utalii Tanzania 2012/13 Media Award zaidi ya Warembo 30 walipanda jukwaani kwa kuelezea mada ya vivutio vya  Mikoa wanayo wakirisha na kisha Majaji wa Shindano hilo kutoka Shule Kuu ya Waandishi wa Habari na mawasiliano ya Umma walitangaza warembo Sita walioingia katika Sita Bora na Baadae waliulizwa Maswali kila mmoja na swali lake na pia swali la pili lilikuwa ni Swali la Jumla ambapo wote waliulizwa. Washiriki wote walijibu kwa umahili na baadae wakapatikana washindi watatu ambapo Mshindi wa kwanza alikuwa ni Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Arusha Rose Godwin, Mshindi wa Pili alikuwa Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Rukwa Neema Kafanunzi na Mshindi wa tatu alikuwa Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Mtwara Baby Juma.
Mshindi wa Tuzo hiyo ya Mshindi wa SMJC Miss Tourism Tanzania 2012/13 Media Award   kutoka Mkoa wa Arusha Rose Godwin Alipata zawadi  ya Udhamini wa kusomeshwa katika Shule Kuu hiyo ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mara baada ya kutoa Tuzo, Rais wa Miss Utalii Tanzania Aliwashukuru Wadhamini wakuu wa Tuzo hiyo ya SJMC Miss Tourism Tanzania 2012/13 Media Awards, ambao ni Shule  Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma kwa kutoa Heshima kubwa ya Kumsomesha Mshindi wa Tuzo hiyo katika chuo hicho na kuongeza kuwa Elimu ndio Ufunguo wa Maisha na Hilo ni Jambo muhimu katika Taifa letu la Tanzania ambapo  Wasomi zaidi wanahitajika ili Kujenga Taifa na Kukuza Uchumi wa nchi yetu.