Skip to main content

RAIS KIKWETE AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KATIKA MAZISHI YA KOCHA ATHUMANI KILAMBO LEOM

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la mchezaji mkongwe wa Yanga na baadaye Kocha wa Pan Africa Marehemu Athumani Kilambo leo Machi 11, 2013 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. Marehemu Kilambo, ambaye alifariki jana usiku baada ya kuugua saratani ya koo kwa takriban miaka miwili,atakumbukwa kama beki imara wa Yanga na Kocha stadi wa Pan Africa ambaye aliiwezesha Klabu hiyo kutwaa ubingwa wa taifa mwaka 1982. Pia amefundisha nyota wengi wa 
kandanda nchini wakiwemo kina Kassim Manara, Adolf Richard, Mohamed Mkweche, Juma Pondamali na wengineo wengi ambao walichezea Taifa Stars kutokea Yanga na Pan.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiondoka baada ya kuongoza maelfu ya waombolezaji katika mazishi ya  mchezaji mkongwe wa Yanga na baadaye Kocha wa Pan Africa Marehemu Athumani Kilambo leo Machi 11, 2013 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa Yanga Lawrence Mwalusako katika mazishi ya  mchezaji mkongwe wa Yanga na baadaye Kocha wa Pan Africa Marehemu Athumani Kilambo
leo Machi 11, 2013 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. wengine toka kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika. Ndugu Adam Malima Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Mhe Ranmadhani Madabida na kulia ni Mwenyekiti wa Yanga Bw. Yusuf Manji.


PICHA NA IKULU

Comments