RAGE AUNGURUMA MSIMBAZI:ASEMA DOLA 300,000 ZA OKWI ZINAWATOA UDENDA WANAOLETA CHOKOCHOKO

 Mwenyekiti  wa Simba Al Hajj Ismail Aden RAge akizungumza na wanachama pamoja na mashabiki wa Simba hii leo mara baada ya kurejea kutoka nchini India alipokwenda kwa ajili ya matibabu.
 Baadhi ya mashabiki wakimsikiliza Rage


 Baadhi ya mashabiki wakimsikiliza Rage

 Baadhi ya mashabiki wakimsikiliza Rage

 Baadhi ya mashabiki wakimsikiliza Rage


Baadhi ya mashabiki wakimsikiliza Rage

Na Dina Ismail
MWENYEKITI wa klabu ya Simba Alhaj Ismail Aden Rage amesema kuwa chokochoko zinazoendelea ndani ya klabu hiyo inatokana na tamaa ya dola 300,000 za mauzo ya aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo Emmanuel Okwi aliyeuzwa katika klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia.
Aidha, Rage amesisitiza kuwa hakuna kitu kinachoitwa mapinduzi ndani ya klabu hiyo na kwamba anawasubiri kwa hamu leo makao makuu ya klabu hiyo wale waliotangaza kumpindua.
Akizuingumza na mashabiki na wanachama wa klabu hiyo jioni ya leo makao makuu ya klabu mitaa ya Msimbazi na Twiga mara baada ya kurejea kutoka nchini India alipokwenda kwa matibabu, Rage alisema wanaoleta matatizo ndani ya klabu hiyo ni wale wenye utu wa kujil;imbikizia mali.
Alisema chini ya uongozi wake Simba imefanya mambo ya uwazi na ukweli ikiwamo hilo suala la kuuza wachezaji ambapo fedha zimeonekana tofauti na waliomtangulia kwani walipowuza wachezaji ferdha ziliyeyuka.
“Tumemuuza Samata (Mbwana) , tumemuuza Ochan (Patrick) fedha zimeoonekana lakini je wao walipowauza kina Henry Joseph, Haruna Moshi (Boban), Danny Mrwanda, na wengineo klabu ilipata sh ngapi?
Rage aliongeza kuwa chini ya uongozi wake wamewezesha kupatikana kwa fedha kupitia kodi ya pango ya jengo hilo ambapo awali ilikuwa sh 200,000 lakini sasa imepanda hadi milioni 2 na hiyo pia ni sababu inayowapa tamaa watu hao weasioitakia mema.
Akienda mbali zaidi Rage alisema kama kundi hilo lililofanya mapinduzi lingekuwa halali hata watu wqaliowateua kuongoza kwa muda Zacharia Hans Poppe na Rahma Al Kharoos ‘Malikia wa Nyuki’ wasingewakatalia kukalia hayo madaraka yao ya muda.
 Rage alisema kwa sasa uongozi umedhamirtia kuiletea mafanikio timu hiyo kongwe kama huku akisema ni aibu kwa hali iliyonayo pamoja na ukongwe huo ukilinganishga na Azam hayo jana kwenye makao makuu ya klabu hiyo mara baada ya kuwasili kutoka nchini India alipokwenda kwa ajili ya matibabu.
“Angalia Azam ina miaka 10 tu katika ulimwengu wa soka ina mafanikio makubwa, lakini Siumba ina miaka 70 hakuna cha maana tyulichofanya lazima tuone aibu,”aliongeza
Hivi karibuni zaidi ya mashabiki 700 wa timu hiyo waliitisha mkutano mkuu wa dharula na kuadhimia kumng’oa Rage na wenzake kwa madai ya kushindwa kuiongoza klabu hiyo kiasi cha kufanya timu ya Simba kufanya vibaya kwenye mechi zake za Ligi Kuu ya Vodacom kabla ya kutolewa katika hatua ya pili ya kombe la Shirikisho barani Afrika.