PAMOJA
na kutojulikana sana hapa nchini lakini ubora alionao bondia Pascal Ndomba
maarufu kama ‘Kimondo’ amefanikiwa kupata ulaji nchini Marekani.
Kimondo
bondia mwenye makazi yake nchini Martekani amelamba dili ya kufanya kazi kwa
miaka minne katika kampuni ya Nelson Promotion ya Miami, nchini Marekani.
Katika
mahojiano na mwandishi wa makala haya, Kimondo pamoja na kumshuru mungu anasema
atafanya jitihada zote kuhakikisha anaipeperesha vema bendera ya Tanzania.
Anasema
kwa muda mrefu amekuwa na ndoto za kuipeperusha bendera ya Tanzania kupitia
mchezo huo, hivyo kwa nafasi aliyoipata hatofanya makosa.
Kimondo
anasema alipata dili hilo baada ya mmliki wa kampuni hiyo kumshuhudia akizipiga
na Mrusi Issa Akberbaew lililofanyika Urusi mwaka 2011 na kudundwa.
“Mpinzani
wangu alinizidi uzito ndiyo maana aliweza kushinda, hata hivyo Nelson Promotion
waliridhishwa na kiwango change na kuondelea kunifuatilia zaidi katika
mapambono tofauti’, anasema.
Bondia
huyo anasema kuwa alikipiga na Agron De
Zilla wa Uswisi na kuchapwa katika pambano lililofanyika Uswisi na bada ya hapo
wamiliki wa Nelson Promotion walimfuata na kutaka kufanya naye kazi.
Anaongeza
kuwa baada ya kukubaliana na kampuni hiyo alitakiwa kujiunga na kituo chao
maalum cha mazoezi kilichopo Marekani ambapo huko alikutana na mabondia kutoka
nchi tofauiti kama Mexico, Cuba, Marekani na nyinginezo.
Akiwa
huko pamoja na mazoezi pia alikuwa akipatia lishe maalum ambayo itamuzesha
kupungua uzito ili kufikia unaotakiwa na aliweza kupungua kutoka kilo 81 hadi
kufikia kilo 72.
“Yaani
kule ni mazoezi tu na pia kuna wataalamu wanaosimamia lishe ili kumfanya bondia
apate uzito unaostahili,”anaongeza.
Anasema
baada ya uongozi kuridhishwa na kiwango alichofikia katika kituo hicho ikiwemo
kupungua uzito, alifanyiwa vipimo vya afya na baada ya kuonekana yupo fit ndipo
walipomsainisha makataba wa kufanya nae kazi.
Kimondo
anasema baada ya kupata dili hilo anatarajiwa kupanda ulingoni kwa mara ya
kwanza Aprili 20 mwaka huu katika ulingo wa MGM huko Florida, Marekani kukwaana
na bondia wa huko katika pambano lisilo la ubingwa.
“Mpambano
huo utakuwa wa uzito wa Middle Kilo 72,
na kwa sasa ninaendelea kujifua ili niweze kuishinda mpambano
huo,”anasema.
Anaongeza
kuwa atacheza kwanza mapambano kadhaa ya kujipima uwezo na mabondia wa huko
kabla baadaye ya kuanza kuwania ubingwa wa dunia unaotambuliwa na vyama vya WBC
na WBA.
Akizungumzia
hali ya mchezo huo hapa nchini, Kimondo anasema umekuwa ukishuka kutokana na
mabondia wale wale kupigana kila siku sambamba na kutojitosa kuwania mataji
makubwa.
Anasema
mabondia wengi wamekuwa waoga wa kucheza na mabondia wengine ikiwemo yeye kwa
kuhofu kupigwa na kupoteza heshima zao hali ambayo haiwasaii kitu katika medani
hiyo.
“Kila
siku ni Cheka (Francis), Nyilawila (Karama), Maugo (Mada), Kaseba (Japhet)
hakuna wengine wapya, sasa hii haiwasidii kituy na inaonesha ni waoga wa
kuthubutu kucheza na wengine, “anasema.
Kimondo
anasema kwa kudhihirtisha kauli yake baadhi ya mabondia wamekuwa wakikwepa
kuzipiga naye na kutoa visingizoi kibao yote nmi hofu ya kupigwa na kupoiteza
sifa zao.
Akiwa
na matarajio ya kufika mbali zaidi katika medani hiyo, Kimondo anawashauri
mabondia wenzake kujituma kwa kufanya mazoezi ya kutosha badala ya kutafuta
umaarufu kupitia vyombo vya habari.
“Wasipigane
kwa kuzoeaa , tunataka bingwa wa kweli na si bora bingwa,’anasema Kimondo.
Aidha,
Kimondo anamshukuru mmiliki wa kampuni ya mabasi ya Sumry, Humud Mohammed
Summry ambapo amekuwa akifanya kazi kama msimamizi na kusema kuwa bossi huyo
amekuwa akimsaidia sana katika jitihada zake za kujiendeleza katika mchezo huo.
KIMONDO
NI NANI:
Jina
la kimondo lilitokana na uzito wa ngumi zake ambapo alipewa mwanzoni mwa miaka
ya 2000 alipokipiga na Joseph Marwa katika moja ya pambano lililoandaliwa na
kampuni ya Dynamite chini ya Shomary Kimbau.
Na
aliitwa Kimondo baaada ya Sayari moja kuanguka mkoani Mbeya ambapo ndipo asili ya Kimondo katika miaka ya
2000.
Akiwa
ni mzaliwa wa Kyela mkoani Mbeya,Kimondo
alikuwa akiupenda mchezo huo tangua akiwa mdogo na hiyo inatokana na kuvutiwa
na bondia bingwa wa zamani wa uzito wa juu duniani, Mike Tyson.
Baada
ya kumaliza shule alijibidiisha katika kujifunza mchezo huo chini ya Mwalimu
Jordan Mwanjelwa na kisha Omary Yazidu kabla ya kutua mikononi mwa Said Tambwe
ambaye alimuzesha kuwa bondia mahiri.
Kimondo
aliwahi kutwaa ubingwa wa Afrika Masharik na Katika mwaka 2011 kwa kumtwanga
Mkenya Moses Odhiambo katika pambano la uzito wa Super Middle.
Aidha,
Kimondo amewako kuzidunda na Fike Wilson, Rashid Matumla, MAneno Oswald ‘Mtambo
wa Gongo’ na kutoshana nguvu, huku akimtandika Karama Nyilawila.
Maoni:dinazubeiry@gmail.com
au tembelea http: dinaismail.blogspot.com
Comments
Post a Comment