PAMBANO LA KUMPONGEZA CHEKA MOROGORO LAFUTWA


Mapambano ya mchezo wa ngumi kumpongeza bondia Francis Cheka 'SMG' yaliyopangwa kufanyika Machi 16, mwaka huu, katika ukumbi wa Vijana Social, mjini hapa, yamefutwa.
Akizungumza na mtandao huu, mratibu wa mapambano hayo, Andrew Mtabazi alisema mapambano hayo yamefutwa baada ya kukosekana kwa wadhamini.
Mtabazi alisema waandaaji walikuwa na kiasi kidogo cha fedha hivyo waliitaji sapoti zaidi lakini amedai hakuna wafadhili waliojitokeza licha ya kuwafuata wadau mbalimbali wa michezo mkoani Morogoro ili waweze kusaidia.
Alisema kufuatia hali hiyo wameamua kufuta mapambano hayo na kuendelea na mipango yao mingine.
“Tulikuwa na lengo zuri tu la kumpongeza Cheka kwa mafanikio aliyopata katika mchezo wa ngumi lakini wadau wengine wameshindwa kutuunga mkono hivyo tumeamua kuachana na mpango huo”, alisema.

Comments