MEDIA DAY KUFANYIKA VIWANJA VYA LEADERS APRILI 6

Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari asubuhi ya leo kwenye ukumbi wa City Sports Lounge, Dar es Salaam kuhusu udhamini wa kampuni yake kwenye tamasha la Waandishi wa Habari, Media Day Bonanza lililopangwa kufanyika Aprili 6, mwaka huu kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Amir Mhando na kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TASWA, Grace Hoka.