MALKIA WA NYUKI APASUA JIPU:ASEMA HAUNGI MKONO KUNDI LOLOTE KWANI AKILI YAKE NI KUIPATIA MAFANIKIO TIMU YA SIMBA


MAKAMU Mwenyekiti wa kamati maalum ya kuisimamia klabu ya Simba, Rahma Al Kharoos ‘Malkia wa Nyuki’ amesema hayuko tayari kufanya kazi na kundi lolote ndani ya klabu ya Simba na kwamba akili yake ipo katika kuiwezesha timu ifanye vizuri kwenye mechi zake za ligi ili iweze kupata nafasi za juu.
Al Kharoos ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa kamati ya fedha ya Simba amelazimika kutoa kauli hiyo kufuatia baadhi ya wanachama wa klabu hiyo kuung’oa uongozi wa klabu hiyo chini ya mwenyekiti wake, Alhaj Ismail Aden Rage na kumteua yeye pamoja na Zachari Hanspope kuongoza kwa muda.
Hata hivyo, Hanspope ambaye alikuwa ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya Simba kabla ya kubwaga manyanga hivi karibuni, alikataa utezi huo na kusema anaheshimu katika ya klabu hiyo.
Akizungumza kwa simu leo kutoka nchini Uingereza, Al Kharoos alisema hayupo upande wowote ndani ya klabu hiyo kwani uwepo wake Simba ni katika kuisaidia timu hiyo ifanye vizuri katika kwenye michezo yake iliyosalia.
Alisema kwa kuendeleza malumbano ambayo hayana tija na matokeo yake wanaweza kujikuta timu inapotea zaidi kwenye ligi na mwisho wa siku wanakosa wa kumlaumu.
Aicha Al Kharoos aliongeza kwa kitu muhimu kwake ni kuisaidia timu na si kuongoza na kama uongozi utakuja baadaye, hivyo anachokingalia kwa sasa ni mustakabali mzima wa timu hiyo.
“Sipo upande wa harusi wala talaka mimi ninaangalia zaidi mafanikio ya timu nataka timu iopande hadi nafasi ya pili na huwezi jua inaweza ikatokea miujiza na kushika hata nafasi ya kwanza,”alisema
“Pamoja na kuwa nipo safari ninamawasiliano ya karibu sana na benchji la ufundi ili kuwapa hamasa katika utendaji wao...hapa akili zetu ni kushinda kwanza mechui zetu za kule Kanda ya ziwa tukiuanza na Kagera Sugar na baadaye Toto African,”aliongeza Alkharoos.

Comments