Na Mwandishi Wetu
JUMLA ya warembo 23 wamejitokeza kushiriki katika shindano
la kumtafuta Miss Tabata 2013 ambalo litazinduliwa siku ya Pasaka kwenye ukumbi
wa Da’ West Park Tabata.
Mratibu wa shindano hilo ,
Godfrey Kalinga alisema jana warembo hao watatambulishwa pamoja na wale
wanaoshiriki Miss Mzizima siku ya sikukuu ya Pasaka Da West Park.
Kalinga aliwataja warembo waliojitokeza kuwania taji la Miss
Tabata 2013 na kuendelea na mazoezi Da West Park ni Martha Gewe (19), Zilpha
Christopher (19), Hidaya David (22), Aneth Ndumbalo (19), Amina Ally (18),
Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19), Kazunde Kitereja (19), Angela Fradius (19), Domina Soka (21), Rehema
Kihinja (20), Glory Jigge (18) na Sophia Claud (21).
Aliwataja wengine ni Lilian Mpakani (19), Lilian Msanchu
(19), Rita Frank (20), Pasilida Mandali (21), Rachel Mussa (19), Jasmin Damian
(18), Angelina Mkinga (19), Mercy Mwakasungu (20), Tunu Hamis (19), Blath
Chambia (23), Ray Issa (22), Shamim Abass (22) na Shan Abass (22).
Utambulisho wa warembo hao, utasindikizwa na burudani
kabambe kutoka bendi ya Twanga Pepeta “Wazee wa Kisigino”.
Kapinga alisema wapenzi wa tasnia ya urembo Jijini Dar es
Salaam, watapata fursa ya kuwaona warembo kabla ya Miss Tabata kufanyika Mei
mwaka huu.
Miss Tabata 2013 imedhaminiwa na Konyagi, CXC Africa,
Fredito Entertainment na Saluti5 na kuandaliwa na Bob Entertainment na Keen
Arts.
Washindi watano kutoka Tabata watafuzu kushiriki Miss Ilala
baadaye mwaka huu.
Anayeshikilia taji la Miss Tabata ni Noela Michael ambaye
pia ni Miss Ilala.
Comments
Post a Comment