KINA SAMATA NA WACHEZAJI WA AZAM FC WAIKAMILISHA STARS


KIKOSI cha Stars kilichopo kambini kujindaa na mchezo huo kimekamilika baada ya wachezaji wake Mbwana Samata, Thomas Ulimwengu na wengine kutoka Azam Fc kuripoti kambini. 
Samata na Ulimwengu wanaokipiga katika klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) walijiunga na wenzao jana jioni, huku wachezaji wengine wa Azam Fc John Bocco, Mwadini Ally, Aishi Manula na Hamisi Mcha walijiunga jana.Wachezaji hao wote walikuwa wakizichezea timu zao wikiendi iliyopita katika michuano ya kimataifa. 
Wambura alisema kwamba, Stars  inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ikiwa chini ya Kocha Kim Poulsen  inaendelea na mazoezi yake kwenye Uwanja wa Taifa.