KIM KUTANGA KIKOSI KITAKACHOIVAA MOROCCO KESHO


Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Kim Poulsen anatarajia kesho (Machi 13 mwaka huu) kutaja kikosi chake kitakachoivaa Morocco.
Mkutano huo wa Waandishi wa Habari utafanyika saa 5 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Morocco kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Machi 24 mwaka huu.