KIBANDA APELEKWA AFRIKA KUSINI, TASWA YALAANI SHAMBULIO LAKE


 Makamu mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Theophil Makunga pamoja na wakili wa kujitegemea Juvenalis Ngowi wakimjulia hali Kibanda mchana wa leo katika taasisi ya mifupa (MOI)
WAKATI mhariri mtendaji wa kampuni ya New Habari Corparation, Absalom Kibanda akipelekwa nchini Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu zaidi,chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania (TASWA) kimeungana na waandishi wa habari wote kulaani kitendo cha watu wasiojulikana kumvamia na kumjeruhi vibaya Kibanda.
Kibanda ambaye pia ni mwenyekiti wa jukwaa la wahariri, alikutwa na mkasa huo usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake Mbezi Beach jijini Dar es salaam wakati akirejea kutoka kazini.
Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa New Habari Corparation Hussein  Bashe, wavamizi hao ambao hawakuiba wala kupora kitu chochote, walimjeruhi vibaya Kibanda sehemu za kichwani, huku poia wakimn'goa meno kadhaa, kumkata kidole na kumchoma na kitu chenye ncha kali jicho lake la kushoto.
n Bashee alisema tukio hiyo ni la kusikitisha na  halikupaswa kutokea kwani hakuna mwenye haki ya kumhukumu binadamu mwnzake.
 Alisema kuwa pamoja na jitihada za madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili bado wameshauriwa kumpeleka Afrika Kusini kwa ajili ya uchunguzi zaidi katika jicho lake ambalo linaonekana kupata athari zaidi kuliko sehemu yeyote ya mwili wake.
Katika hatua nyingine, TASWA kupitia kwa mwenyekiti wake Juma Pinto imeeleza kusikitishwa na tukio hilo na kusema 

ingependa kuona watu ambao wamehusika na tukio hilo kukamatwa ili sheria ichukue mkondo wake,sisi Kama waandishi tungeomba vyombo vya ulinzi na Usalama vifanye kazi yake kwa uadilifu mkubwa.Hatua hiyo italeta moyo wa Imani ambao waandishi sasa wameingiwa na wasiwasi mkubwa juu ya maisha yao.

Tusingependa Kama waandishi kuamini yanayosemwa lakini kutokana na uadilifu mkubwa wa vyombo vyetu vya ulinzi na Usalama kuwapata watu ambao wamehusika na tukio hilo.

Sisi tunaamini tukio hili la mwenzetu kuvamiwa na watu hao halikuwa kwa bahati mbaya ni Jambo ambalo linaonekana Kama limepangwa na Kama ni hivyo lengo na madhumuni yake ni nini kwa waandishi wa Tanzania? Uhuru na Usalama wa waandishi upo wapi?

Katakana na tukio hili la mpiganaji na Kiongozi wetu kuvamiwa ,ipo haja ya sisi waandishi kuungana pamoja katika kutafuta Usalama wetu.kuna matukio mengi ya waandishi yametokea na tumekuwa tukipiga kelele lakini matokeo yake hakuna hatua ambazo serikali inayafanyia kazi.

Katakana na majeraha maki wa aliyopata mwenzetu,tunaiomba serikali na hats Mheshimiwa Rais,Dr Jakaya Kikwete kutoa Masada wa mwenzetu kwenda kutibiwa nje,tunaamini serikali ni sikivu na Rais wetu ni mwenyeji kusikia kilio cha watu wake.

Kibanda na wenzak ndani ya Jukwaa la wahariri wamekuwa mstari wa mbele katika kurudisha hadhi ya tasnia ya habari na kujenga umoja miongoni mwa waandishi wa habari na kuifanya tasnia ya habari kuheshimika tofouti na ilivyokiwa nyuma.

Tunaungana na kampuni ya habari, wafanayakazi wenzak, familia yake na waandishi wote kwa jumla na kumuomba mungu ampomye ili tuweze kuunganae nae katika kusaidia kupasha habari Watanzania lakini ili aweze kuwaongoza waandishi wenzake.