AZAM FC YAZIDI KUIKIMBIZA YANGA


USHINDI wa bao 1- 0 iliyoupata Azam Fc leo dhidi ya  Ruvu Shooting umeifanya izidi kuikimbiza vinara wa ligi hiyo, Yanga Sc ambao leo wamelazimisha sare tasa na maafande wa polisi Morogoro.
Katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Mabatiti, Mlandizi, Pwani, Kipre Tchetche ndiye aliiapatia bao la ushindi hivyo kuifanya kufikisha pointi 43, huku Yanga ikiongoza kwa pointi 49.
Mbali na mchezo , mchezo mwingine wa ligi hiyo uliokuwa kati ya Kagera Sugar dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo Kagera imeshinda mabao 2-1, mchezo ulipigwa dimba la Kaitaba, Kagera.
African Lyon nayo imshinda 1-0 dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
 Aidha, JKT Oljoro imewatandika maafande wenzao JKT Ruvu mabao 2-0, mchezo uliopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha