AZAM FC WATIMKIA SUDAN


WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye kombe la Shirikisho barani Afrika, Azam Fc wameondoka alfajiri ya leo kuelekea Sudan Kusini tayari kwa mechi ya marudiani dhidi ya wenyeji , Al Nasri Juba ya huko utakaopigwa kesho.

Kikosi cha Azam chini ya kocha wake Stewart Hall kimeondoka na matumaini makubwa ya kuhakikisha kinashinda mechi ya kesho kama ilivyokuwa mchezo wa awali uliopigwa nyumbani wiki iliyopita na kushinda mabao 3-2, hivyo inahitaji sare ya aina yoyote ili kusonga mbele.

Kikosi cha Azam kilichoondoka leo ni pamoja na
 makipa: MWADINI ALLY na AISHI SALUM MANUEL.

Mabeki ; JOACKINS ATUDO, LUCKSON KAKOLAKI, DAVID MWANTIKA, WAZIRI SALUM, HIMID MAO na MALIKA NDEULE.

Viungo; KIPRE BOLOU, JABIR AZIZI, IBRAHIM MWAIPOPO, SALUM ABOUBAKARY 'SURE BOY', HUMPHREY MIENO, ABDI KASSIM 'BABI' na KHAMIS MCHA 'VIALI'
.
Washambuliaji; JOHN BOCCO 'ADBAYOR', KIPRE TCHETCHE, BRIAN UMONY, SEIF ABDALLAH na GAUDENCY MWAIKIMBA.