YANGA WAINGIA KAMBINI KATIKATI YA JIJI


VIEWED 367 TIMES

Kikosi cha Young Africans
Baada ya kuichapa timua ya Azam FC kwa bao 1-0 mwishoni mwa wiki, timu ya Young Africans Sports Club leo imeingia kambini katika Hoteli ya Tansoma katikati ya jiji kujiaandaa na mechi inayofuata dhidi ya timu ya Kagera Sugar, mchezo utakaofanyika siku ya jumatano katika dimba la Uwanja wa Taifa kuanzia majira ya saa 10 jioni.
Young Africans ambayo iliwapa furaha washabiki, wapenzi wa soka na wanachama wake kwa soka safi la ufundi wa hali ya juu, itashuka dimbani kuwakabili wakata miwa hao ambao katika mchezo wa awal waliibuka na ushindi wa bao 1-0 mchezo uliofanyika katika dimba la Kaitaba mjini Bukoba.
Young Africans yenye jumla ya point 39 na mabao 34 ya kufunga na mabao 12 ya kufungwa itashuka dimba la uwanja wa Taifa kuhakikisha inaibuka na ushindi katika mchezo huo ili kuendelea kuongoza  msimamo wa Ligi Kuu ya VPL na hatimaye iweze kutwaa Ubingwa huo.
Mara baada ya mazoezi ya leo asubuhi, kocha mkuu Brandts amesema anashukuru vijana wake kwa kufanya kile alichowaagiza, nidhamu ya hali ya juu na kushika maelekezo yake ndio vitu vilivyopelekea kuendelea kuibuka na ushindi katika michezo mbali mbali waliyocheza.
Nawapongeza washabiki, wanachama na wapenzi wa Yanga waliojitokeza kwa wingi siku ya jumamosi, kuja kuwashangilia vijana, kikubwa nawaomba waendelee na moyo huo huou kwani waliwapa nguvu vijana na kuwafanya wacheze kwa kujiamini mda wote wa mchezo 'alisema Brandts'.
Aidha Brandts alisema matokeo ya juzi yameendelea kuiweka Yanga katika nafasi nzuri ya kuelekea kutwaa Ubingwa na atahakikisha wanajitahidi kushinda kila mchezo ili kujiweka katika mazingia mazuri ya kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Kikosi cha  wachezaji 26 na benchi la ufundi wote wameingia kambini katika Hoteli ya Tansoma mara baada ya mazoezi ya leo asubuhi na wachezaji wote ni wazima kiafya na kiakili hivyo hakuna mcheaji hata mmoja ambaye ni majeruhi.
CHANZO:www.youngafricans.co.tz