YANGA SC WAENDELEA KUJIANDAA NA VPL

Kikosi cha timu ya Young Africans leo kimeenndelea na mazoezi katika katika uwanja wa mabatini Kijitonyama kujiandaa na mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi ya Vodacom dhidi ya timu ya African Lyon siku ya jumatano Februari 13 ,2013 katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Wachezaji wote wamefanya mazoezi leo chini ya kocha Ernest Brandts na kocha msaidizi Fred Felix Minziro kwa ajli ya mchezo huo huku habari njema ikiwa ni kurejeea dimbani kwa mlinzi wa kushoto Oscar Joshua ambaye alikuwa majeruhu kufuatia kupata maumivu ya enka katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar mwishoni mwa wiki.imu z
Kufuatia wachezaji nane (8) kuitwa kuzitumikia timu za taifa kwa ajili ya michezo ya kujipima nguvu leo, kocha Brandts amewaita wachezaji wanne (4) kutoka kikosi cha U-20 kwa ajili ya kufanya mazoezi pamoja na kikosi cha kwanza.
Wachezaji walioanza mazoezi jana asubuhi ni Notikely Masasi, Issa Ngao, Benson Michael na Abdullahman Sembwana wote wakiwa ni wachezaji wa kikosi cha U-20.
Kelvin Yondani, Athumani Idd, Frank Domayo, Saimon Msuva na Nadir Haroub mara baada ya mchezo wa kimataifa leo dhidi ya Cameroon kesho watajiunga na wachezaji wenzao katika maozezi ya asubuhi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo ujao dhidi ya African Lyon.
Aidha wachezaji Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite (Rwanda) na Hamis Kiiza (Uganda) na kocha wa makipa (Razaki Siwa) wanatarajiwa kuanza kurejea kesho baada ya kuzitumikia timu zao za Taifa tayari kabisa kuendelea na maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu siku ya jumatano. 

Comments