Mechi namba 119 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa juzi
(Februari 13 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam na kumalizika kwa Yanga kuibuka ushindi wa
mabao 4-0 imeingiza sh. 68,438,000.
Watazamaji 12,147 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo
iliyochezwa kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000
huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 16,170,252.45 wakati Kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 10,439,694.92.
Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi
ambapo 10,982 walikata tiketi hizo na kuingiza sh. 54,910,000.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh.
8,222,162.26, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 4,933,297.36, Kamati
ya Ligi sh. 4,933,297.36, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
2,466,648.68 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,918,504.53.
Comments
Post a Comment