Wambura akiwaonesha waandishi wa habari moja ya gazeti lililoandika kuhusu kujiuzulu kwake BMT mwaka 2001
Baadhi ya wanahabari wakimsikiliza Wambura hii leo.
IWAPO
Tanzania itafungiwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), ama kutokea
mgogoro wowote utakaoathiri soka la Tanzania basi Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF)
Leodger Tenga ndiye atapaswa kulaumiwa , imefahamika.
Aidha, Tenga
ametakiwa kuwaomba radhi wadau wa soka nchini kwa kuwa alikosea na kukiuka
katiba ya TFF katika kufanya mabadiliko au marekebisho ya Katiba kwa
kutoitisha Mkutano Mkuu amnbao una
mamlaka ya kufanya mabadiliko ya katiba hiyo. Hayo yamesema leo jijini Dar es
Salaam na aliyekuwa mgombea wa nafasi ya makamu wa Rais wa TFF, Michael
Wambura alipozungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari
(Maelezo).
Alisema kwa
kuwa tayari serikali imeshatoa uamuzi wake kuhusiana na mustakabali mzima wa
uchaguzi huo analazimika kuamini Tenga na kamati yake watatii na kutekeleza
uamuzi huo na hasa ikizingatiwa kuwa
ndani ya kamati hiyo kuna wajumbe ambao ni watumishi wa serikali.Watumishi hao
wa serikali ni pamoja na Athuman Nyamlani (Mahakama), Cresentius Magori (NSSF),
Athuman Kambi (Tanroad) na Wallace Karia (TAMISEMI).
“Kwa kwenda
kinyume na maamuzi ya serikali itakuwa ni utovu mkubwa wa nidhamu, hinyo
napenda kuwasihi na kuwashauri ili
wajipime na kujitathmini wakati wakijadili utekelezaji wa maamuzi ya
Serikali,”alisema .
Wambura
alienda mbali na kusema kwamba anashindwa kuelewa na kuamini msimamo wa
Tenga kwani kama ni mtu mwenye
kumbukumbu nzuri mwaka 2001 wakati anajiuzulu nafasi ya Makamu wa Mwenyekiti
wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) akiwa anzungumza na waandishi wa Habari
march, 2001 alijaribu kuwaonesha Watanznia kuwa yeye ni muumini wa kufuata
sheria na taratibu zilizopo.
“hatuna budi
kutekeleza majukumu yetu kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo kinyume
chake ni vurugu, pale tunapoona sheria yetu inapitwa na wakati na haifai
inatulazimu tukubaliane kuifanyia mabadiliko kabla hatujaacha kuiheshimu,”L.C
Tenga (2001).
…hivyo ni
wazi Tenga anafahjamu kuwa kwenda kinyume na utaratibu halali uliowekwa wa
mabadiliko ya kAtiba ya TFF mwishowe huleta vurugu kama ambavyo Falasafa yake
inavyomuelekeza, kwa mantiki hiyo anatulazimisha Watanzania kuamini mkanganyiko
huu uliopo sasa Tenga anaufahamu mapema na alishiriki na kuruhusu hali hiyo
itokee kwa msalahi yake binafsi,”alisema Wambura.
Wambura
alisema Tenga katika mkutano wake na waandishi wa habari alieleza moja ya
sababu za kujiuzulu kwake nafasi ya makamu Mwenyekiti wa BMT ni kupinga uamuzi
wa serikali wa kukubaliana na FIFA kuhusu uundwaji wa kamati ya mpito ya FAT
kwa madai kwa kufanya hivyo serikali itakuwa imepoteza uwezo wa kusimamia vyama
vya michezo nchini.
…kukubali
kutekeleza agizo la FIFA kama ilivyo amuliwa na serikali ni kuzitekeleza
taratibu na sheria za nchi, serikali inajivua madaraka ya udhibiti wa vyma vya
michezo vya kitaifa na kulikabidhi jukumu hilo kwa vyma vya michezo vya
kimtaifa.Haiwezekani tufanye hivyo na hakuna nchi yoyote makini inayofanya
hivyo”, Tenga 2001.
Kama hiyo
haitoshi Wambura ameshauri baadhi ya mambo kwa kamati ya Utendaji kwa lengo la
kunusuru soka la Tanzania kuingia katika
mgogoro mpya, TFF iridhie kutekeleza
uamauzi wa Serikali bila kigugumizi.
“TFF itangaze
tarehe mpya na mchakato wa uchaguzi, pia kutokana na kuwepo kwa mashauri mawili
katika mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza na Tanga, TFF ikutane na
walalamikaji ili mashauri yamalizike nje ya mahakama kwani hata kama FIFA watakuja uchaguzi
hauwezi kufanyika kwa kuwa tayari kuna zuyio la muda kusimamisha uchaguzi uliotolewa na Mahakama
Kuu Kanda ya Tanzania”
“Ili haki
itendeke wale wote walioomba na watakaooomba kugombea nafasi mbalimbali
waruhusiwe na wapitishwe ili wapiga kura waamue kiongozi wanaomtaka, pia
mabadiliko ya katika yangoje uongozi mpya utakaoingia madarakani ili nao waone
na kuchambua mapungufu na kuyarekebisha,”
“Kwa kuwa
kamati ya uchaguzi muda wake wa kukaa ofisini kikatiba ni miaka miwili ni wazi
muda wao utakuwa umefikia ukomo ni vema ukaandaliwa utaratibu wa muda ili
ipatikane kamati itakayosimamia uchaguzi huo, pia katika kuendesha na kusimamia
uchaguzi huo kanuni za uchaguzi zilizotumika katika uchaguzi wa 2008 zitumike”
Wambura pia
ameitaka kamati ya utendaji itoe tamko la kumuwajibiusha katibu mkuu wa TFF
Angetile Osia kwa utovu wa nidhamu kwa kutoa matamshi ya kejeli dhidi ya waziri
mwenye dhamana ya kusimaia michezo.
“Baada ya
kufanya haya niliyoyapendekeza TFF iitaarifu FIFA kuwa Tanzania imetatua
mgogoro wake yenyewe na hivyo kuiondoa katika orodha ya aibu ya nchi ambazo
haziwezi kuandaa na kusimia chaguzi zake bila usimamizi wa FIFA,”aliongeza.
Comments
Post a Comment