WALETE WALETE LIBOLO-LIEWIG


TIMU ya Simba, kesho inaanza kampeni ya michuano ya kimataifa kwa kuwakaribisha mabingwa wa soka wa Angola, timu ya Recreativo de Libolo katika mechi ya kwanza ya hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kocha mkuu wa Simba,  Mfaransa Patrick Liewig, alisema kikosi chake kipo imara na tayari kuanza vizuri kampeni hiyo ya kimataifa
Alisema anashukuru wachezaji wake kuwa wenye afya njema na ari kubwa kuelekea mechi hiyo, hivyo anaamini watapata matokeo mazuri.
Liewig alisema pamoja na ugumu wa mechi hiyo kutokana na ubora wa timu za Angola dimbani, lakini wamejipanga kupata ushindi kujiweka nafasi nzuri kabla kurudiana.
“Vijana wangu wapo tayari kuwakabili wapinzani wetu Libolo, wameahidi kucheza kwa juhudi kubwa ili kushinda na kujiweka kwenye nafasi nzuri kabla ya kurudiana, tunaomba sapoti ya Watanzania,” alisema.
Naye Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ambaye ni Kocha Msaidizi, amewasihi wapenzi na mashabiki wa soka kujitokeza na kuishangilia Simba katika mechi ya kesho.