SIR NATURE, INSPECTOR HAROUN KUSINDIKIZA PAMBANO LA SIMBA NA WASUDAN


 Inspector Haroun
Sir Nature

WASANII wakongwe wa bongo Fleva kutoka pande za TMK, Haruna Kahena 'Inspector Haroun' na Juma Kiroboto 'Sir Nature' wanatarajiwa kutoa burudani wakati wa mchezo wa kombe la Shirikisho baina ya Azam Fc na Alnasir Juba ya Sudan Kusini.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa jumamosi kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni.
Aidha viingilio katika mchezo huo ni sh 2,000 kwa viti vya  kijani na Bluu, huku  mashabviki watakaokaa viti vya Orange watalipa sh 5,000 wakati watakaokaa VIP C na B watalipa  sh 10,000 na VIP A watalipa sh 20,000..