SIMBA YAWAKUTA YA AZAM FC

NDOTO za Simba kutetea ubingwa wa ligi kuu bara zunezidi kutoweka baada ya leo kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Mtibwa Sugar ya Turiani, Morogoro.
Katika mchezo wa ligi hiyo uliopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa, Salvatory Ntebe ndiye alitikisa nyavu za Simba na kuifanya Mtibwa Sugar iendeleze ubabe wake kwa Simba katika msimu huu wa ligi kwani katika duru la kwanza iliilaza mabao 2-0.
Kwa mantiki hiyo kipigo ilichokipata Simba leo kinafanana na kile walichokipata wanalambalamba Azam Fc dhidi ya yanga ambapo pia walitandikwa bao 1-0.