SIMBA SC YAREJEA DAR, KIINGILIO MECHI YAO NA LIBOLO BUKU TANO TU


WAKATI kikosi cha Simba kinatarajiwa kuwasili kesho kutoka Arusha kilipokuwa kimepiga kambi, kiingilio cha chini cha mchezo wake wa ligi ya mabingwa dhidi ya Recretivo de Libolo ya angola kimepangwa kuwa sh.5,000.                                                                                                                                                                                                                                           
Timu hizo zinatarajiwa kukwaana jumapili kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo kiingilio hicho kitahusisha mashabiki watakaokaa viti vya rangi ya kijani na bluu.
 Ofisa  habri wa Simba Ezekiel Kamwaga alisema kwamba kikosi cha timu hiyo mara baada ya kurejea Dar es Salam leo kitaingia kambini kwenye hoteli ya Spice iliyopo katika ya jiji kuendelea na maandalizi yake.
Alisema wachezaji wote ukiacha majeruhi Felix Sunzu na Paul Ngalemwa wao majeruhi, wapo katika hali nzuri na jana asubuhi walifanya mazoezi ya mwisho huku jioni wakipewa mapumziko.
Kamwaga aliongeza kuwa kwa sasa kikosi kipo tayari kwa mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa na hasa ikizingatiwa kuwa wapinzani wao nao wamejipanga vema, lakini watahakikisha wanashinda.
Aidha, Kamwaga alivitaja viingilio vingine ni sh 10,000 kwa watakjaokaa viti vya rangi ya chungwa, sh 15,000 kwa watakaokaa VIP C, sh 20,000 kwa VIP B na sh 30, kwa VIP A.