SIMBA SC WAITISHA MKUTANO MKUU WA DHARULA KUJADILI VIPIGO


KAMATI ya utendaji ya klabu ya Simba imeazimia kuitisha mkutanio mkuu wa dharura wa klabu hiyo ambao utakuwa na ajenda moja tu ya kujadili mwenendo mbaya wa klabu hiyo kwenye ligi kuu ya Vodacom. 
Ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema leo kwamba kamati ya utendaji ya Simba iliyokutana jana  usiku imepitisha uamuzi wa kuitishwa kwa mkutano huo ili kujadili hali hiyo. 
Alisema wanatarajiwa kutangaza tarehe na mahala utakapofanyika mkutano huo wakati wowote kuanzia sasa na kwamba uongozi umewataka wanachama wa klabu hiyo kusuusubiria mkutano huo. 
“Uongozi pia umesikitishwa na sintofahamu inayoendelea ndani ya klabu yetu na hasa katika michezo yake ya ligi kuu hivyo basi  uongozi umekubaliana kuitisha mkutano mkuu wa dharula ili kuweza kutafuta ufumbuzi wa hali hii,”alisema.