SIMBA SC KWENDA ANGOLA ALHAMIS

MABINGWA wa ligi Kuu soka Tanzania Bara, Simba Sc wanatarajiwa kwenda nchini Angola alhamisi ya wiki ijayo tayari kwa mchezo wao wa marudiano wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Recreativo do Libolo ya huko itakayopigwa Machi 4.
Katika mchezo wa kwanza ulipigwa jijini Dar es Salaam wiki iliyopita, Simba ililala kwa bao 1-0.