ONGEA NA JANET TALK SHOO CHAWAFARIJI WATOTO WANAOLELEWA KITUO CHA KIWOHEDE

Mwendeshaji wa Kipindi cha Ongea na Janeth kinachorusshwa na Clouds Tv na DStv Bi. Janeth Sostenesi akisaini daftari la wageni katika kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Kiwohede kilichopo Buguruni jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili kwa ajili kufurahi na watoto hao katika sikukuu ya wapendanao pamoja na kukabidhi msaada.
Bi. Janeth Sostenesi akijaribu moja ya bidhaa za mikono zinazotengenezwa na watoto wa kituo cha Kiwohede. Kushoto Mratibu Mipango wa Kituo hicho Bi. Stella Mwambenja.
Mkurugenzi Mkuu wa kituo cha Kiwohede Bi. Justa Mwaituka akizungumza na Mtangazaji wa Kipindi cha Ongea na Janeth pamoja Crew nzima inayotengeneza kipindi hicho kuhusiana na maendeleo yaliyokwisha fikiwa mpaka sasa na mipango ya baadae ya kuboresha mazingira ya kituo hicho.
Mtangazaji wa kipindi cha Ongea na Janet na crew yake wakiimbia na kufurahi pamoja na watoto wa kituo cha Kiwohede siku ta Valentines Day.
Mkurugenzi Mkuu wa kituo hicho akitambulisha wageni kwa watoto wanaolelewa kituoni hapo.
Mmoja wa watoto wanaolelewa na kituo hspo akitoa shukrani kwa Bi. Janeth Sostenese pamoja na Crew kwa kuonyesha upendo wa dhati kitu ambacho ni adimu kwao kutokana na mazingira waliyotoka.
Mtangazaji wa Kipindi cha Ongea na Janet akizungumza na watoto wa kituo cha Kiwohede ambapo amewataka kudumisha upendo baina yao na kujiona kama watu wengine, pia amewaasa kukazania elimu ambayo itawakomboa na kuweza kuwa kama yeye hapo baadae na amewaahidi kuendelea kuwa nao pamoja.
Janeth Sostenesi na Crew nzima ya Ongea na Janeth wakikabidhi msaada wa fedha taslim kwa mwakilishi wa watoto hao ikiwa ni upendo wake katika siku hii ya wapendanao.
Baadhi ya Watoto wa kituo cha Kiwohede wakifurahia msaada huo kutoka kwa kipindi cha Ongea na Janeth.
Crew nzima ya Ongea na Janeth katika picha ya pamoja na watoto wanaoishi katika mazingira magumu wa kituo cha Kiwohede.
Janeth Sostenesi akishow love na Mkurugenzi Mkuu wa shirikila lisilo la kiserikali la Kiwohede Bi. Justa Mwaituka.

Comments