MECHI YA MARUDIANO YA SIMBA NA LIBOLO SASA KUPIGWA J'2


KIKOSI cha kosi cha timu hiyo kinatarajiwa kuondoka Ijumaa alfajiri kuelekea Luanda, Angola kwa ajili ya mchezo wake wa klabu bingwa ya Afrika dhidi ya wenyeji Recreativo do Libolo ya huko utakaopigwa jumapili katika mji wa Calulo nchini humo. 
Kikosi cha wachezaji 20 na viongozi saba wa Simba wakiongozwa na mwenyekitii wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hanspoppe pamoja na mjumbe wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Mohsin Balhabou ndicho kitakachokwenda Angola. 
Hata hivyo Kamwaga alisema awali mchezo huo ambao ulikuwa upigwe jumamosi mjini Luanda sasa utapigwa jumapili mjini Caculo ambapo umbali kutoa Luanda hadi Caculo ni masaa manne,hivyo wameandika barua kwa wenyeji wao kuomba wapatiwe usafiri wa ndege kwa mujibu wa sheria na kanuni za Shirikisho la Soka Afrika (CAF).