MALKIA WA NYUKI AHIMIZA WANAWAKE KUJITOKEZA KWA WINGI KESHO KUISHANGILIA SIMBA

MFADHILI wa Simba Rahma Al Kharoos 'Malkia wa Nyuki' amewaomba mashabiki na hasa wanawake kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa TAifa kesho kwa ajili ya kwenda kuishangilia Simba itakapokipiga na Recreativo de Libolo ya Angola katika mchezo wa klabu bingwa ya Afrika.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Rahma alisema michezo ni furaha, undugu na amani hivyo hata wanawake hawana budi kujikeza kwa wingi uwanjani hapo ili kuipa sapoti Simba katika mchezo huo.
Aliongeza kuwa Simba inaiwakilisha Tanzania hivyo mashabiki hawana budi kuachana na siasa za Usimba na Uyanga kwa kuungana pamoja kuishangilia ili kuwapa nguvu vijana.
"Nimengumza na vijana wana morari ya hali ya juu sasa shime wadau na hasa kina mama mjitokeze kwa wingi siku ya jumapili,"alisema Rahma ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya fedha ya Simba.