MALINZI AWAUNGANISHA SIMBA, YANGA...WATISHIA KUMWAGA DAMU, WAMNG'ATA SIKIO RAIS KIKWETE

Baadhi ya mashabiki na wanachama wa Simba na Yanga wakizungumza na waandishi wa habari leo kuhusiana na hatua watakazozichua baada ya kuenguliwa katika kinyang'aro cha uchaguzi wa TFF, Jamal Malinzi.Kutoka kushoto ni Salum Mkemi, Suleiman Kato an Kaisi Edwin.


WANACHAMA na  mashabiki wa soka nchini wameapa kuandamana na kwenda mahakamani kuzuia kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), baada ya kamati ya Rufaa ya Shirikisho hilo kumuengua mgombea wa nafasi ya urais, Jamal Emil Malinzi.
Aidha, wanachama hao kutoka vilabu vya Simba, Yanga na Azam wamemtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete kuingilia kati suala la kuenguliwa kwa Malinzi kwani limefanywa kwa chuki binafsi likiwa na lengo la kumbemba mpinzani wake, Athuman SIKU moja baada ya kamati Nyamlani.
Wakizungumza na waandishi wa habari leo, pamoja na kupinga kuondolewa kwa Malinzi, wametoa siku tatu kwa TFF kumrejesha katika kinyang’anyiro hicho, kinyume na hapo watakwenda kudai haki yao mahakamani.
Mmoja ya wadau hao Kaisi Edwin alisema kwamba kanuni za Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) chombo cha mwisho cha maamuzi ni Mahakama yas Usuluhishi wa Migogoro ya Michezo (CAS) lakini TFF haijaelekeza baada ya kamati ya Rufaa chombo kipi kinaweza kutoa suluhu ya masuala kama hayo.
 Alisema walitaka kupata changamoto mpya ya uongozi kupitia kwa Malinzi lakiini kitendo cha kumuengua kunaonesha ni jinsi gani wanavyotaka kuendelea kuwa na watu wasiotaka maendeleo ya soka.
“Ni bora tufungiwe na FIFA, tunajua maslahi wanayoyapata TFF na tutatoa uozo wote...kwa hili hata damu itamwagika na kwa gharama yoyote tutahakikisha uchaguzi haufanyiki kama wasipomrejesha Malinzi labda waende kufanyia Geneva,”aliusema Kaisi.
Naye Suleiman Kato alisema anashangazwa na kamati ya Rufaa kumuengua Malinzi kwa madai ya kutokuwa na uzoezfu wakati alipitishwa kugombea uchaguzi wa mwaka 2008 inagawa alishindwa kwa kura chache na rais wa sasa wa TFF, Leodger Tenga.
“Malinzi pia nia mwenyekiti wa chama cha soka Kagera sasa iweje apitishe kugombea huko na mpaka anapata kiti hicho nah ii leo mseme hana uzoefu na uongozi wa soka, kinachoonekana hapa ni kutaka kudidimiza soka la Tanzania, hilo hatulikubali,”alisema.
Mdau mwingine, Mgeni Ramadhan ‘Dogo Macho’ alisema inaonesha wazi wazi wanataka viongozi kwa ajili ya maslahi binafsi kitu ambacho si sahihi kwani Watanzania wanaopenda soka wanataka maendeleo na si viongozi maslahi.
“Naamini Rais kikwete ambaye ni mpenda michezo atasikia kilio hiki na kuingilia kati, kuna watu wapo kwa ajili ya kubebwa, huyo Nyamlani anatoka Kusini, kuna mwanakamati mmoja Murtaza mangungu ambaye ni Mbunge anambeba, pia kuna mwingine aliwahi kuwa Hakimu wa Temeke na nyamlani akiwa karani wake,”alisema.
Kwa upande wake, mdau mwingine Said Bakari alisema kuwa wataanza kuonesha hasira zao kuanzia leo kwenye uwanja wa Taifa kwenye mechi baina ya Yanga na African Lyon, kabla ya kuendelea na hatua yao katika michezo ya kimataifa ya timu za Simba na Azam wikiendi hii.
“Huyu malinzi anabebwa kwani tunajua mwenyekiti wa kamati alikuwa wakati akiwa Hakimu temeke yeyealikuwa karani, Mangungu naye pamoja na kumpigia debe ni jirani na baba yake Nyamlkani,”alisema.
Wadau hao kwa pamoja wamepaza sauti hizo baada kamati ya Rufaa ya TFF kumuengua Malinzi katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika februari 24 mwaka huu ambapo kwa mujibu wa ratiba kampeni zinatarajiwa kuanza leo.
Katika hatua nyingine, Malinzi kesho anatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari kuhusiana na sakata hilo.