(TAAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI)
CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA)
kimefuta wazo la kuendesha mdahalo kwa wagombea wa nafasi za juu za uongozi wa Shirikisho la
Soka Tanzania
(TFF).
Mdahalo huo ulikuwa ufanyike Februari 15, 2013 na tayari
chama kilikuwa katika hatua nzuri ya mazungumzo na wadhamini pamoja na kituo
kimoja cha televisheni kwa ajili ya kurusha 'live' tukio hilo , ambapo kesho ilikuwa tutangaze
utaratibu mzima wa mdahalo huo.
Katika mazungumzo ya leo na uongozi wa kituo hicho ambao
hautaki tukitangaze, tumekubaliana kufuta wazo la mdahalo kwa sababu nafasi ya urais amebaki mgombea mmoja,
hivyo mdahalo hautakuwa na tija.
Dhamira ya awali ya kufanya mdahalo ilikuwa kuwapa fursa
wapiga kura wasikie vyema sera za wagombea urais na Makamu wa Rais, ili
wananchi wawasikilize wagombea hao na pia wapiga kura wawatambue vizuri.
Hata hivyo TASWA itatafuta utaratibu mwingine mzuri ambao
utawezesha wagombea kuzungumza na waandishi wa habari na kuulizwa maswali
mbalimbali ambayo tunaamini kwa kiasi fulani yatasaidia wapiga kura katika
uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Februari 24 mwaka huu. TASWA inawatakia kila la
kheri wagombea wote wa TFF waliobakia.
TASWA imekuwa ikifanya mdahalo kwa wagombea wa nafasi za juu
kwenye uchaguzi wa TFF, ilifanya hivyo mwaka 2001 na mwaka 2004 ingawa haukuwa
wa live, ikafanya wa live mwaka 2008, ambapo yote ilikuwa ya mafanikio makubwa.
Nawasilisha.
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
12/02/2013
Comments
Post a Comment