JULIO AWAPASHA YANGA, KUONGOZA LIGI SI UBINGWA: SUNZU MAJERUHI

Julio na Kamwaga
KOCHA msaidizi wa Simba Jamhuri Kihwelo 'Julio' amewapasha mahasimu wao Yanga kwamba kuongoza kwao kwenye ligi kuu ya Vodaconm si kwamba watatwaa ubingwa.
Akizungumza jijini dar es Salaam leo, Julio alisema wana deni la pointi sita ili kuwafikia Yanga ambapo tatu watazipata keshokutwa kwa JKT Ruvu na tatu nyingibne kwa Azam Fc.
Alisema kikosi chake kipo katika hali nzuri kikichochewa na kambi waliyoifanya nchini Oman hivyo anamini watafanya vema katika michezo yao na kutetea ubingwa wao.
Simba ambayo ilianza mzunguko wa pili wiki iliyopita kwa kuitanmdika African Lyon mabao 3-1, katika mchezo wa keshokutwa itamkosa mshambuliaji wake wa kimtaifa Mzambia Felix Sunzu anayekabiliwa na majeruhi.