JAMAL MALINZI AEMGULIWA UCHAGUZI WA TFF

KAMATI ya Rufaa ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), jana imemuengua Mwenyekiti wa Chama cha Soka Kagera (KRFA), Jamal Malinzi kugombea Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Taarifa ya TFF jana, imesema kwamba Wengine walioenguliwa ni Michael Wambura aliyekuwa akiwania nafasi ya Makamu wa Rais na Ahmed Yahya aliyekuwa akiwania nafasi ya Uenyekiti wa Bodi ya Ligi.
 pekee aliyepitishwa katika nafasi ya Urais, inayoachwa wazi na Leodegar Tenga ni Athumani NyamlaniMalinzi aaliwekewa pingamizi Agape Fue, ambaye awali alishindwa na kuamua kukata rufaa.

.Nyamlani amepeta kuelekea uchaguzi huo, utakaofanyika Februari 24, mwaka huu kwa sababu pingamizi alilowekewa limetupiliwa mbali.