FFU WA NGOMA AFRICA BAND WAJICHIMBIA KUJIANDA NA VITA YA 'KUZIBA NYUFA'


Habari za uhakika tena nyeti vimevuja kutoka katika kambi ya bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" aka FFU yenye makazi  yake nchini Ujerumani.

Kuwa bendi hiyo inayofanananishwa na kikosi kazi FFU imeingia kambini katika msimu  wa barafu huko ughaibuni,
kwa kujifua na kujiandaa kwa kuwaletea washabiki vitu vipya ! 
Pia Kiongozi wa bendi hiyo Kamanda Ras Makunja
mwanamuziki mwenye mjina mengi ya kutisha tisha kama vile kamanda wa FFU,Kolokoloni namba 1,mfalme
Hui Hui wa gagagigikoko n.k,kamanda alikaririwa  mwanzoni mwa Januari2013 kuwa Bendi hiyo inaenda kambini
Kujiandaa na vita ! alipoulizwa vita gani? alijibu vita vipya vya "KUZIBA NYUFA" zilezojitokeza katika jamii yetu!

Ndio kusema Kamanda wetu wa FFU Ras Makunja kaingia kambini na kikosi chake kujiandaa na vita?
vita venyewe vya kuziba nyufa na mimomonyoko au mipasuko katika jamii yetu! kauli ya kamanda Ras Makunja
inaonekana inadarubini ya mtazamo mkali unaoona mbali! katika mahojiano na jarida la africa analysis la Uingereza,

Ni siku chache tu bendi hiyo yenye tabia za ki-FFU ilionekana katika uwanja wa ndege wa Bremen,wakiwa wanaondoka lakini wakusema wapi wanako elekea, "wanamuziki wa bendi hiyo wakiwa na mizigo" nyusoni wakiwa seriously tena  hawakuwa tayari kujibu chochote wanachoulizwa ! tena katika msimu wa baridi na barafu wanaenda kambini? tena haijulikani nchi gani?
kama Serbia au Bosnia ? pengine Israel ! hakuna anayejua !

Kamanda Ras Makunja na ffu wa Ngoma Africa Band wapo kambini,kwa kujiandaa na vita vya kuziba nyufa, na mwaka huu pia bendi hiyo inatimiza miaka 20 tangu izaliwe mwaka
1993 hadi mwaka huu 2013 ni umri mkubwa.

Washabiki wanasubiri kwa hamu kubwa kuona na kujiunga na na vita vilivyotangazwa na bendi hiyo chini ya kamanda
Ras Makunja mwenye kichwa kigumu au mkuu wa "Watoto wa Mbwa" Ngoma
Africa ukipenda FFU .
wasikilize at http://www.ngoma-africa.com au www.ngoma-africa.com