TIMU ya Azam FC, imeanza vema kampeni ya michuano
ya kimataifa kwa ushindi wa
mabao 3-1 dhidi ya
Al Nasr Juba ya Sudan Kusini,
mechi iliyopigwa
kwenye Uwanja wa Taifa,
jijini Dar es Salaam .
Ushindi huo sio tu faraja kwa
wapenzi na mashabiki wa timu hiyo, bali kwa Watanzania hasa ikizingatia ndio mara ya kwanza kucheza
michuano ya kimataifa.
Azam Fc ilikuwa ya kwanza kupata bao katika
dakika ya 14, likifungwa na Abdi Kassim ‘Babi.’
Al
Nasri walisawazisha dakika ya 39, likifungwa na
Fabian Elias kutokana mpira wa krosi ya
Kone James.
Katika mechi hiyo
iliyochezeshwa na mwamuzi Davies Omweno wa Kenya , mashabiki wa Yanga
walishangilia Al Nasir na kuwakebehi watani
zao Simba kuelekea mechi ya leo dhidi ya Libolo ya Angola .
Azam walionekana kuja na
nguvu zaidi katika kipindi cha pili kwani dakika ya 80, Kipre Tche akaifungia
bao la pili akiunganisha krosi ya Hamis Mcha aliyekuwa mwiba.
Tcheche alirejea
kwenye nyavu za Al Nasr na kuifungia timu yake bao la tatu, hivyo kufanya
kuvuna ushindi wa mabao 3-1.
Comments
Post a Comment