AZAM FC, JUBA KURUDIANA MACHI 3


MCHEZO wa marudiano wa kombe la Shirikisho baina ya Azam Fc na Al Nasir Juba ya Sudan Kusini unatarajiwa kupigwa Machi 3 mwaka huu, imefahamika. 
Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Boniface Wambura alisema kwamba, wamepokea barua kutoka chama cha soka cha nchi hiyo na kuwapa taarifa hizo. 
Alisema mchezo huo unatarajiwa kupigwa katika dimba la Juba Stadium, huko Sudan Kusini kuanzia saa 11.30 jioni kwa saa za hapa nyumbani. 
Katika mchezo wa awali uliopigwa hapa nchini wiki iliyopita Azam ilishinda mabao 3-1, hivyo wenyeji wanahitaji kushinda mabao 2-0 ili kusonga mbele.