Wachezaji wa Yanga wakishangilia
Kikosi cha YAnga
Kikosi cha Black Leopards
MABINGWA wa
soka Afrika Mashariki na Kati, Yanga, leo wam evuna ushindi wa mabao 3-2 dhidi
ya Black Leopards ya Afrika Kusini katika mechi ya kirafiki ya kimataifa
iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Yanga
wakicheza mechi ya kwanza tangu warejee nchini wakitokea Uturuki walikokuwa
wamepiga kambi ya wiki mbili kujiandaa na raundi ya pili ya Ligi Kuu Bara,
walionesha kiwango cha kuvutia hasa kipindi cha kwanza huku Jerry Tegete
‘Mturuki,’ Simon Msuva na Haruna
Niyonzima waking’ara zaidi.
Tegete
alikuwa wa kwanza kuwainua katika viti mashabiki wa Yanga baada ya kuifungia
bao kwa mkwaju wa penalti dakika ya 30, iliyotolewa na mwamuzi Hashimu Abdallah
baada ya Niyonzima kuangushwa na beki Humphrey Khoza wa Leopards.
Katika
kipindi cha kwanza, Yanga walitawala kwa
kiasi kikubwa huku Frank Domayo na Athumani Idd ‘Chuji’ wakikamata vema dimba
huku Edger Manaka wa Leopards kumpunguza kasi Domayo kwa kumchezea rafu za mara
kwa mara.
Dakika ya 13,
nusura Yanga wapate bao kwa mpira uliotokana na free kick iliyopigwa na Joshua
na kwenda nje sentimita chache langoni mwa Leopards, hivyo hadi timu hizo
zinakwenda mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha
pili kilianza kwa kasi kwa timu zote kufanya mabadiko kadhaa na kusaka mabao
zaidi, hivyo dakika ya 46, Khoza aliisawazishia timu yake bao kwa kichwa
akiunganisha mpira wa kona uliokuwa umepigwa na Rodney Ramagalela.
Mabadiliko ya
nyota wawili kila upannde mwanzoni mwa kipindi cha pili yalionekana
kuidhoofisha Yanga huku Leopards wakionekana kucheza soka ya kutulia zaidi.
Katika mabadiliko hayo, Yanga iliwatoa mapacha Kabange na Mbuyu Twite na
kuingiza Simon Msuva na Juma Abdul.
Wageni
Leopards iliwatoa Thomas Madimba na Edger Manake na kuwaingiza Mahlatse Maake
na Karabo Tshepe na dakika ya 59, Domayo aliifungia Yanga bao la pili kwa shuti
dhaifu ndani ya boksi baada ya mgongeo mzuri wa Msuva na Niyonzima.
Dakika ya 64,
Tegete ambaye mashabiki wamempachika jina la Mturuki kutokana na kung’ara
katika ziara ya hivi karibuni nchini humo
akiifungia mabao mawili katika mechi mbili tofauti, aliifungia Yanga bao
la tatu akimalizia krosi ya Msuva na kuamsha shngwe za mashabiki.
Kutokana na
kuonesha kiwango cha kuvutia, Tegete alishangiliwa kwa muda wote wa mchezo huo
wa jana hadi pale alipotoka kumpisha George Banda na Dakika ya 88, Leopards
walipata bao la pili kwa mkwaju wa penalti likifungwa na Ramagalela baada ya
nyota huyo kuangushwa na Juma Abdul.
Yanga:Ali
Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin
Yondan, Athuman Iddy ‘Chuji’, KAbange Twite, Frank Domayo, Jerry Tegete
‘Mturuki’, Didier Kavumbagu na Haruna Niyonzima
Leopards: Ayanda
Mishali, Ernort Dzaga, Nkosiyabo Xakane, Harry Nyirenda, Humphrey Khoza,
Munganga Djunga Jean, Mongezi Bobe, Thoimas Madimba, Abbas Amidu, Edger Manaka
na Rodney Ramagalela
Comments
Post a Comment