YANGA YA UTURUKI UTAIPENDA, YAITANDIKA TENA BLACK LEOPARDS

MABINGWA wa Afrika Mashariki na Kati , Yanga Sc wameendelea kuonesha walichokovuna nchini Uturuki baada ya leo kuitandika kwa mara nyingine Black Leopards ya Afrika Kusini katika mchezo uliofanyika klwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Awali, Yanga ambayo ilikuwa nchini Uturuki kwa kambi maalum iliwabanjua Wasauzi hao mabao mabao 3-2 katika mechi ya kwanza iliyopigwa jumamosi iliyopita kwenye uwanja wa Taifa jijini dar es Salaam.
Katika mchezo wa leo ambao Yanga ilionekana kucheza kitimu na umaridadi mkubwa mabao yake yalipachikwa na Said Bahanuzi 'Spider Man' na Jerry Tegete 'Mturuki'.