YANGA WAJIFUA KWA MARA YA MWISHO UTURUKI


Wachezaji wa Young Africans, Juma Abdul, Said Bahanuzi & Didier wakifanya mazoezi ya Gym leo asubuhi katika Hotel ya Fame Residence
Timu ya  Young Africans leo asubuhi imemaliza mazoezi  yake kwa kufanya mazoezi ya kujenga mwili na uimara (Gym) iliyopo katika hoteli ya Fame Residence leo asubuhi na yakiwa ndio mazoezi ya mwisho katika kambi ya mafunzo ya wiki mbili iliyokuwa ikiendelea katika viwanja vya Fame Residence Football mijini Antlaya.

Kocha mkuu Ernest Brandts akishirikiana na Fred Felix Mizniro na Razaki Siwa leo waliongoza mazoezi ya Gym kuanzia majira ya saa tatu na nusu asubuhi mpaka majira ya saa saa tano na nusu asubuhi ambapo baada ya mazoezi hayo wachezaji wamepewa nafasi ya kupumzika kujiandaa na safari ya hapo kesho kurudi Tanzania.
 
Akiongelea michezo ya kirafiki mitatu waliocheza na timu za Armini Bielefeld, Deinizlispor na Emmen Fc kocha mkuu wa Yanga Ernest Brandts amesema michezo ilikuwa ni mizuri na wamepata nafasi ya kuona mapungufu machache yaliyojitokeza na anaamini watayafanyia kazi na kuendelea kufanya vizuri.
 
Tumecheza michezo mitatu, wa kwanza tulitoka sare na Amrinia Bielefeleld, mchezo ulikua mzuri na timu yangu ilicheza vizuri kwa dakika 90 zote za  mchezo licha ya Arminia kusawaisha bao dakika za lala salama huku mwamuzi aklishindwa kutoa maamuzi sawa na mshika kibendera wake, ambapo mfungaji alikua maeotea.
 
Mchezo wa pili dhidi ya Denizlispor nao pia timu ilicheza vizuri na kuweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini umakini wa washambuliaji ulitukosesha ushindi kwani Tegete alitumia nafasi aliyoipta kufunga bao la mapema kabla ya Waturuki hawajasawazisha kwa bao la utata  kisha kupewa penati ya utata pia.
 
Mchezo wa mwisho dhidi ya Emmen FC ulikuwa mzuri pia na kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza tuliutawala mchezo na kupata nafasi kadhaa za kufunga mabao lakini kutokua makini wa washambuliaji wetu pia kulichangia sisi kukosa ushindi, kabla ya kipindi cha pili Emmen FC kucharuka na kupata mabo mawili ya haraka haraka kutokana na uzembe wa walinzi na mlinda mlango Yusuph abDUL
 
Tunaushukuru uongozi kwa kukubali kutupa nafasi ya kuweka kambi Uturuki, tumkeaa pamoja kwa mda mrefu huku tukitoka mafunzo kwa vitendo, vifaa na mahitaji yote vikiwepo ,kukiwa na hali ya utulivu, kifupi tumejifunza mambomengi sana ya msingi ambayo yatatusaidia kufanya vizuri katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom na mashindano yatakayotukabili alisema 'Brandts'
Ally Mustafa 'Barthez, na Nizar Khalfani wakifanya mazoezi ya Gym leo asubuhi katika hoteli ya Fame Residence
CHANZO:www.Youngafricans.co.tz