YANGA SC YAENDELEA KUJIFUA UTURUKI


Wachezaji wa Young Africans wakiwa katika mazoezini katika ufukwe wa Fame Residencxe
Kikosi cha Young Africans Sports Club kimeendelea na mazoezi yake leo katika uwanja wa Fame Residece Football uliopo Antalya kisha jioni timu ikaenda kufanya mazoezi katika ufukwe wa bahari, eneo lililopo nyuma ya hoteli Fame Residence ikiwa ni siku ya tatu katika ziara ya mafunzo nchini Uturuki kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom.
Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga mholanzi Ernie Brandts amesema anafurahishwa na maendeleo ya kambi, kwani toka wameanza mazoezi jumatatu leo ni siku ya tatu wakiwa nchini Uturuki na anaona mabadiliko makubwa kwa wachezaji wake, huku akisema hofu iliyokuwepo kwa watanzania juu ya hali hewa ya baridi kali si kweli kwani hali ya hewa katika mjii huu ni baridi kiasi tu na hata leo katika mazoezi ya asubuhi palikuwa na jua.

Wachezaji wanaendelea kuzoea mazingira, na kujifunza mambo mengi yanayohusu soka kwani wageni mbalimbali waliofika katika mji huu wamekuwa wakipenda kujua mengi kuhusiana na timu ya Young Africans na soka la Tanzania kwa ujumla.

Wachezaji wakiwa mazoezini Ufukweni
Majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki timu ilifanya mazoezi ya ufukweni katika ufukwle wa Hotelu ya Fame Residence  pemebezoni mwa Bahari ya Mediteranian.

Kocha wa makipa wa timu ya Bayern Leverkusen Detier Gansi jioni alishuhudia Young Africans ikifanya mazoezi ya ufukweni ambapo alisema amefurahia kuifahamu timu ya Yanga na wachezaji wake wanaonekana kuwa na morali ya kucheza soka, hivyo anaamin ziara hii itaisaidia timu kuwa pamoja na kujiandaa vyema na ligi alisema

Wachezaji wakiwa katika mazoezi ya asubuhi uwanja wa Fame Residence Footbal
Wakati huo huo mchezaji wa kimataifa wa timu ya Taifa ya Rwanda Haruna Niyonzima amewasili jioni hii kuungana na wenzake kufuatia kuchelewa kuunganisha ndege siku ya jumamosi usiku akitokea nchini Rwanda alipokuwa amekwenda kuchezea timu yake ya Taifa.

CHANZO:www.youngafricans.com